MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 12 JANUARI, 2025

SIKU YA BWANA YA 1 KATIKA MAJIRA YA UFUNUO.

 NENO LINALOTUONGOZA NI 

WABATIZWAO NI WARITHI WA UZIMA WA MILELE

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Mgeni waliotufikia kwa cheti Joseph Jackson Mutakumwa toka Usharika wa Moshono Arusha. 

3. Matoleo ya Tarehe 5/01/2025

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Mahudhurio ya ibada ya tarehe 05/01/2025 ilikuwa ni washarika 771. Sunday School 56

5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 mchana. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV.

6. Uongozi wa Umoja wa Wanawake, unapenda kuwakumbusha washarika waliochukua bahasha za michango kwa ajili ya kuwalipia ada watoto yatima waweze kukamilisha ahadi zao ili watoto waendelee na masomo yao. Mungu awabariki sana.

7. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana hapo nje na kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=. 

8. Uongozi wa Usharika unapenda kuwataarifu kuwa mafundisho ya watoto wa Kipaimara mwaka 2025 yataanza Jumamosi ijayo tarehe 18/01/2025 saa 3.00 asubuhi hadi saa 5.00 asubuhi. Wazazi mnaombwa sana ushirikiano wenu.

9. Kwaya ya AGAPE, wanatarajia kwenda kuwatembelea watoto wenye tatizo la mgongo wazi katika hospitali ya Taifa - Muhimbili, pamoja na watoto wenye uhitaji wanaolelewa katika kituo cha watoto KIBAHA CHILDREN VILLAGE CENTRE mkoa wa Pwani, January 2025. Kila mwaka kwaya ya Agape hutoa huduma hii na wanapenda kuwashukuru sana washarika wote waliojitoa kwa ajili ya huduma iliyopita. Hivyo wanaomba sana washarika kuwaunga mkono kwa kuchangia huduma hiyo. Unaweza kuchangia fedha taslimu, nguo, mafuta ya ngozi, sabuni za kufulia na kuogea, madaftari, kalamu, maji ya kunywa, dawa za meno au chochote utakachobarikiwa na Mungu. Tafadhali wasilisha sadaka yako ofisi ya Usharika au unaweza kutuma sadaka yako kupitia Account no. 3874006021 jina AGAPE EVANGELICAL SINGER AZANIA FRONT Maendeleo Bank. Mungu wa Mbinguni awabariki sana.

10. Umoja wa Wanawake Azania Front watakuwa na Mkutano Mkuu utakaofanyika tarehe 18.01.2025, siku ya Jumamosi asubuhi saa 3.00 kamili. Kutakuwepo na Neno la Mungu litakalofundishwa na Mchungaji Ipyana. Pia Taarifa ya Fedha na taarifa ya Utendaji zitatolewa.

11. Shukrani: Tarehe 19.01.2025 Umoja wa Wanawake Azania Front watamtolea Mungu Sadaka ya Shukrani kwa mambo makubwa aliyowantedea. Shukrani hii itatolewa na wanawake wote katika ibada zote tatu.

12. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

  • Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Bwana na Bibi Shanny Mbogolo 
  • Upanga: Kwa Bwana na Bibi William Sabaya  
  • Oysterbay/Masaki: Kwa Capt. na Bibi J. Mkonyi

13. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Pili  

Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.