Date:
25-11-2024
Reading:
Ufunuo wa Yohana 1:17-20
Jumatatu asubuhi tarehe 25.11.2024
Ufunuo wa Yohana 1:17-20
[17]Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,
[18]na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.
[19]Basi, uyaandike mambo hayo uliyoyaona, nayo yaliyopo, na yale yatakayokuwa baada ya hayo.
[20]Siri ya zile nyota saba ulizoziona katika mkono wangu wa kuume, na ya vile vinara saba vya dhahabu. Zile nyota saba ni malaika wa yale makanisa saba; na vile vinara saba ni makanisa saba.
Baada ya maisha haya, uzima wa milele;
Yohana anashuhudia kukutana na Bwana Yesu, akimwambia asiogope. Yohana anazidi kufunuliwa kuwa Bwana Yesu yu hai siku zote. Ndiye aliyekufa na kufufuka. Ni hatua ya awali wakati Yohana anaanza kupata Ufunuo.
Yesu anaendelea kujidhihirisha kwetu leo, kwamba yeye ndiye Mwokozi. Ndiye mwanzo na mwisho. Ni wito wangu kwako asubuhi hii kujitoa kwa Bwana Yesu, ukidumu katika Imani ya kweli, ili kuuendea uzima wa ulimwengu ujao. Amina
Siku njema.
Heri Buberwa