Date:
15-11-2024
Reading:
Ayubu 23:10-12
Ijumaa asubuhi tarehe 15.11.2024
Ayubu 23:10-12
10 Lakini yeye aijua njia niendeayo; Akisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu.
11 Mguu wangu umeshikamana sana na hatua zake; Njia yake nimeishika, wala sikukengeuka.
12 Sikurudi nyuma kuiacha amri ya midomo yake; Nimeyatunza maneno ya kinywa chake zaidi ya riziki yangu,
Mwenye kuvumilia hata mwisho ndiye atakayeokoka;
Ayubu anapoendelea kulalamika, anaonyesha ambavyo Bwana hajamuacha. Ayubu anaonyesha kuwa Bwana anazijua njia zake, na ndiye kiongozi wake. Anazidi kukiri kuwa yeye Ayubu amelishika neno la Bwana.
Nini nafasi yetu leo?
Pamoja na yote tunayopitia, tunaongozwa na Bwana? Ni wakati wa kuendelea kukaa na Bwana mioyoni mwetu, awe kiongozi wetu, ili asije akatukana siku ya mwisho, yaani tusikose kuingia katika ufalme wake. Amina
Siku njema
Heri Buberwa