MATANGAZO YA USHARIKA  

TAREHE 10 NOVEMBA, 2024

SIKU YA BWANA YA 3 KABLA YA MAJILIO

NENO LINALOTUONGOZA NI

MWENYE KUVUMILIA HATA MWISHO NDIYE ATAKAYEOKOKA

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Mgeni aliyetufikia kwa cheti ni Daniel Mbonjwa toka Usharika wa Bethelehemu Nyakato Mwanza.

3. Matoleo ya Tarehe 03/11/2024

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 mchana. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV.

5. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana hapo nje na kwenye duka letu la vitabu kwa bei yaTsh. 40,000/=. 

6. Kamati ya Afya na Ustawi wa jamii inapenda kuwatangazia kuwa mafundisho ya afya kwa wanafunzi wa Kipaimara kwa Mwaka wa Kwanza na wa pili yatafanyika tarehe 16/11/2024 kuanzia saa 2.00 asubuhi mpaka saa 9.00 alasiri hapa Usharikani. Wale waliopata Kipaimara wenye umri wa miaka 15 pia wanakaribishwa kwenye mafundisho haya. Wazazi na Walezi mnaombwa kuandikisha watoto watakaohudhuria kwa Parish Worker ili kufanya maandalizi haya.

7. Leo tarehe 10/11/2024 ni siku ya ubatizo wa watoto na kurudi kundini. .

8. NDOA: NDOA ZA WASHARIKA 

KWA MARA YA TATU TUNATANGAZA NDOA YA TAREHE 16/11/2024

SAA 9.00 ALASIRI

  • Bw. Festo Stephen Mazuguni na Elizabeth Eliet Senkoro

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu. 

9. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

  • Upanga: Kwa Bi Terri
  • Mjini kati: itafanyika hapa kanisani jumamosi saa 1.00 asubuhi
  • Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Mama Ruth Korosso
  • Kinondoni: Kwa Prof Kulaba
  • Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bw Joseph na Bi Vupe Mpuya
  • Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach: Watatangaziana
  • Ilala, Chang’ombe, Buguruni: Kwa Bwana na Bi James Monyo
  • Oysterbay, Masaki: Kwa Bwana Arch Dudley Mawalla.

10. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Kwanza.  

Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.