Date:
06-11-2024
Reading:
Ufunuo 21:21-22
Jumatano asubuhi tarehe 06.11.2024
Ufunuo wa Yohana 21:21-22
21 Na ile milango kumi na miwili ni lulu kumi na mbili; kila mlango ni lulu moja. Na njia ya mji ni dhahabu safi kama kioo kiangavu.
22 Nami sikuona hekalu ndani yake; kwa maana Bwana Mungu Mwenyezi na Mwana-Kondoo, ndio hekalu lake.
Sisi ni wenyeji wa mbinguni;
Yohana alifunuliwa mbingu mpya kwa ajili ya wateule. Yohana anasema katika mbinguni mpya anauona mji ambao hauhitaji jua wala mwezi kuuangaza, kwa maana Utukufu wa Mungu huutia nuru, na taa yake ni mwana kondoo. Hakuna usiku, na milango haifungwi. Hakiingii kinyonge wala muovu, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima.
Wengi huihubiri Yerusalemu kwa dhana tofauti, baadhi wakiitaja Yerusalemu ya sasa kule Mashariki ya kati. Wengine huhubiri vitisho kuhusu Yerusalem mpya, badala ya kuwakumbusha watu kumcha Bwana ili waingie Yerusalemu mpya. Yerusalemu mpya siyo ya Israeli kule Mashariki ya Kati, bali ni dhana inayoelezea uzima wa milele kwa wote waaminio. Tubu dhambi zako ili uwe mwenyeji wa mbinguni. Amina
Jumatano njema
Heri Buberwa