Date: 
23-10-2024
Reading: 
Mwanzo 32:24-30

Jumatano asubuhi tarehe 23.10.2024

Mwanzo 32:24-30

24 Yakobo akakaa peke yake; na mtu mmoja akashindana naye mweleka hata alfajiri.

25 Naye alipoona ya kuwa hamshindi, alimgusa panapo uvungu wa paja lake; ukateguka uvungu wa paja la Yakobo alipokuwa akishindana naye.

26 Akasema, Niache, niende, maana kunapambazuka. Akasema, Sikuachi, usiponibariki.

27 Akamwuliza, Jina lako n'nani? Akasema, Yakobo.

28 Akamwambia, Jina lako hutaitwa tena Yakobo, ila Israeli, maana umeshindana na Mungu, na watu, nawe umeshinda.

29 Yakobo akamwuliza, akasema, Niambie, tafadhali, jina lako? Akasema, Kwa nini waniuliza jina langu? Akambariki huko.

30 Yakobo akapaita mahali pale, Penueli, maana alisema, Nimeonana na Mungu uso kwa uso, na nafsi yangu imeokoka.

Tuishindanie Imani katika Kristo Yesu;

Yakobo yuko na wake zake, watoto wake na watumishi wake akisafiri, anawavusha wote halafu anabaki peke yake. Anapobaki peke yake inatokea anashindana na mtu kwa mieleka hata alfajiri. Baada ya kuona hamshindi, anamgusa na kutaka ambariki. Yakobo anabarikiwa na kuitwa Israeli maana alishindana na Mungu, na watu, akashinda. Kwa hiyo Yakobo alikutana na Mungu uso kwa uso, na nafsi yake ikaokoka.

Sehemu hii huwa inawapa shida watu wengi;

-Kwamba Mungu ni mtu?

-Mungu alipigana mieleka?

-Ni Mungu gani aliyeshindwa na Yakobo, mwanadamu tu? n.k

Ilikuwa ni njia ya Mungu kukutana na watu wake moja kwa moja wakati ule. Ni Mungu kweli ndiyo maana alitoa baraka kwa Yakobo. Sisi tunakutana na Mungu kwa njia ya Yesu Kristo tunapomwamini na kumpokea maishani. Tusiiache imani hii ili tuwe na mwisho mwema. Amina

Jumatano njema

Heri Buberwa