Date: 
12-10-2024
Reading: 
Waefeso 4:11-14

Jumamosi asubuhi tarehe 12.10.2024

Waefeso 4:11-14

11 Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu;

12 kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe;

13 hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo;

14 ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu.

Nguvu ya Imani katika Yesu Kristo;

Paulo anaandika juu ya umoja katika imani. Paulo anaainisha huduma alizotoa Kristo ili kuujenga mwili wake, lakini akikazia imani katika kuujenga huo mwili wa Kristo. Paulo anasema hakuna utimilifu kwa kila aaminiye pasipokuwa na imani. Ndiyo maana kwa njia hiyo hiyo, anawaambia wanaotumika pamoja kuungana katika imani.

Ukisoma ujumbe wa Paulo unalihusu Kanisa kukaa pamoja na kuitenda kazi ya Mungu kwa umoja. Lakini Paulo anasema katika umoja huo iwepo imani ndipo utimilifu wa Kristo utakuwepo.

Angalia msisitizo huu;

 Waefeso 4:4-6

4 Mwili mmoja, na Roho mmoja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu.
5 Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja.
6 Mungu mmoja, naye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote.

Tusiiache Imani yetu. Amina

Jumamosi njema

Heri Buberwa