Date: 
11-10-2024
Reading: 
Waefeso 3:14-16

Ijumaa asubuhi tarehe 11.10.2024

Waefeso 3:14-16

14 Kwa hiyo nampigia Baba magoti,

15 ambaye kwa jina lake ubaba wote wa mbinguni na wa duniani unaitwa,

16 awajalieni, kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake, kufanywa imara kwa nguvu, kwa kazi ya Roho wake katika utu wa ndani.

Nguvu ya Imani katika Yesu Kristo;

Mtume Paulo anawaandikia watu wa Efeso akionesha ukuu wa Mungu, pale anaposema "nampigia Baba magoti". Anawataka kumcha katika Imani ili wawe imara katika kumtumikia. Ukiendelea kusoma unaona Paulo akikaza kuhusu imani;

Waefeso 3:17

Kristo akae mioyoni mwenu kwa imani mkiwa na shina na msingi katika upendo;

Ujumbe wa Petro asubuhi hii ni kuwa na Imani katika Yesu Kristo, ambaye tukimwamini hutufanya imara katika kumtegemea yeye. Ni kwa njia ya Imani tunaweza kumkaribia Bwana, na pasipo imani hatuwezi kumpendeza. Kumbe imani yetu katika Bwana ndiyo hutuweka kwake hadi uzima wa milele. Amina

Ijumaa njema

Heri Buberwa