Event Date: 
04-10-2024

Siku ya Ijumaa tarehe 04 Oktoba 2024, ulifanyika mkesha wa kusifu na kuabudu (night of praise) katika Usharika wa Kanisa Kuu Azania Front Cathedral. Tukio hili la kipekee na la aina yake ambalo limefanyika kwa awamu ya pili chini ya uratibu wa Umoja wa Vijana wa Usharika, liliongozwa na Mchungaji Joseph Mlaki na kuhudhuriwa na washarika na wageni mbalimbali.

Akitoa neno la utangulizi, Mchungaji Mlaki aliwaasa washiriki kuimba nyimbo za kumtukuza Mungu. “Huenda umekuja na mzigo katika moyo wako au akili yako lakini natamani utakapoondoka hapa, sifa utakazoimba kwa Mungu atashuka na kutuhudumia na atatufungulia njia pia ya namna ya kupambana na changamoto za maisha yetu. Lakini pia kama umekuja na amani moyoni mwako pamoja na shukrani, basi tuondoke tukijua kwamba tumemshukuru na kumsifu Mungu wetu,” alisema Mchungaji Mlaki.

Mkesha huo ulihudhuriwa na kwaya mbalimbali za Usharika na wageni ikiwemo kwaya ya Sound of Victory.

Angalia picha zaidi hapa chini:

Matukio mbalimbali katika picha wakati wa Mkesha wa Kusifu na Kuabudu (Night of Praise) iliyofanyika tarehe 04/10/2024 katika Usharika wa Kanisa Kuu Azania Front. Picha: AZF Media Team

Tazama Tukio Hilo: https://www.youtube.com/watch?v=RCiEs7tOcp4

--------------MWISHO------------------