Date: 
08-10-2024
Reading: 
2 Wakorintho 5:6-9

Jumanne asubuhi tarehe 08.10.2024

2 Wakorintho 5:6-9

6 Basi siku zote tuna moyo mkuu; tena twajua ya kuwa, wakati tuwapo hapa katika mwili, tunakaa mbali na Bwana.

7 (Maana twaenenda kwa imani, si kwa kuona.)

8 Lakini tuna moyo mkuu; nasi tunaona ni afadhali kutokuwamo katika mwili na kukaa pamoja na Bwana.

9 Kwa hiyo, tena, ikiwa tupo hapa, au ikiwa hatupo hapa, twajitahidi kumpendeza yeye.

Nguvu ya Imani katika Yesu Kristo;

Mtume Paulo anawaandikia Wakorintho juu ya kuishi kwa Imani. Sehemu hii ya waraka inatanguliwa na ujumbe ufuatao;

2 Wakorintho 4:16

Kwa hiyo hatulegei; bali ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa, lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku.

Paulo anasema kwamba utu wa nje ukichakaa, ule wa ndani unafanywa upya siku zote kwa sababu ya imani yetu. 

Ndipo Paulo katika somo anakazia kwamba tukiwa katika mwili tunakaa mbali na Bwana. Paulo anasisitiza kuenenda kwa Imani ili kukaa katika Bwana. Msingi wa ujumbe wa Mtume Paulo asubuhi ya leo ni kuenenda kwa Imani. Tuendelee kukaa kwa imani katika Yesu Kristo kama tulivyompokea, ili tuwe na mwisho mwema. Amina

Siku njema

Heri Buberwa