Date: 
23-09-2024
Reading: 
Kumbukumbu la Torati 11:26-28

Jumatatu asubuhi tarehe 23.09.2024

Kumbukumbu la Torati 11:26-28

26 Angalieni, nawawekea mbele yenu hivi leo baraka na laana;

27 baraka ni hapo mtakapoyasikiza maagizo ya Bwana, Mungu wenu, niwaagizayo leo;

28 na laana ni hapo msiposikiza maagizo ya Bwana, Mungu wenu, mkikengeuka katika njia niwaagizayo leo, kwa kuandama miungu mingine msiyoijua.

Uchaguzi wako ndiyo maisha yako;

Mungu alikuwa anaongea na watu wake na kuwaambia waishi vipi. Aliwaelekeza kumwamini na kumtazama yeye katika yote. Somo tulilosoma ni sehemu, ambapo Mungu anawaambia watu wake kuwa amewaweka baraka na laana. Baraka ni pale ambapo wangesikiliza maagizo ya Bwana, na laana ni pale ambapo wasingemsikia Bwana na kuisikiliza miungu mingine. 

Ujumbe tunaopewa asubuhi ya leo ni kumsikiliza Yesu Kristo aliye Mwokozi wa ulimwengu. Tunamsikiliza kwa njia neno lake na Sakramenti. Ni wajibu wako kuchagua, kati ya Mungu na dunia. Tumchague Yesu Kristo aliye Mwokozi wetu, ambaye ametuahidi uzima wa milele. Amina.

Uwe na wiki njema yenye uchaguzi wa busara.

Heri Buberwa