Date: 
05-09-2024
Reading: 
Malaki 2:10

Alhamisi asubuhi 05.09.2024

Malaki 2:10

Je! Sisi sote hatuna Baba mmoja? Mungu aliyetuumba siye mmoja tu? Basi, mbona kila mmoja wetu anamtenda ndugu yake mambo ya hiana, tukilinajisi agano la baba zetu?

Mpende jirani yako;

Nabii Malaki anaandika akieleza kuwa sisi sote ni watoto wa Baba mmoja, sote tumeumbwa na Baba huyo huyo. Anashangaa kuwa ni kwa nini watu walioumbwa na Mungu mmoja wanatendeana hiana.

Nabii Malaki anaendelea kuandika kuwa wote watendao vile watatengwa na Mungu, maana kutopendana ni kuunajisi utakatifu wa Bwana.

Sisi sote tumeumbwa kwa mfano wa Mungu. Hivyo kumchukia mwenzako ni kuuchukia uumbaji wa Mungu. Wawezaje kusema unampenda Mungu wakati humpendi aliyeumbwa kwa mfano wake? Mpende jirani yako kama nafsi yako. Amina

Alhamisi njema

Heri Buberwa