Date: 
02-09-2024
Reading: 
Kutoka 20:26-17

Jumatatu asubuhi tarehe 02.09.2024

Kutoka 20:16-17

16 Usimshuhudie jirani yako uongo.

17 Usiitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako; wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng'ombe wake, wala punda wake, wala cho chote alicho nacho jirani yako.

Mpende jirani yako;

Somo la asubuhi ya leo ni sehemu ya amri kumi za Mungu ambazo Israeli walipewa kuzifuata, wakiwa ni Taifa lake. Amri tulizosoma zinahusu uhusiano uliopo kati ya mtu na mtu, pale anaposema usimshuhudie jirani yako uongo. Mungu anaendelea kuwaambia wasitamani nyumba ya jirani, mke wake (mume wake), mtumwa wake, mjakazi wake, ng'ombe wake, punda wake, wala chochote alicho nacho.

Huwezi kumshuhudia uongo mtu ambaye unampenda. Huwezi kutamani kitu na (au) mali ya mtu unayempenda kwa maana ya kumuonea wivu asiwe na kitu au mali husika. Kwa hiyo amri ya kutomshuhudia jirani yako uongo inamaanisha kumpenda huyo jirani. Amri ya kutotamani mke na mali za jirani yako ni kumpenda jirani yako. Basi nawe mpende jirani yako kama nafsi yako. Amina

Tunakutakia wiki njema yenye upendo kwa jirani.

 

Heri Buberwa