Date: 
30-08-2024
Reading: 
Mithali 19:21-23

Ijumaa asubuhi tarehe 30.08.2024

Mithali 19:21-23

21 Mna hila nyingi moyoni mwa mtu; Lakini shauri la Bwana ndilo litakalosimama.

22 Haja ya mwanadamu ni hisani yake; Ni afadhali maskini kuliko mwongo.

23 Kumcha Bwana huelekea uhai; Atakaa ameshiba; hatajiliwa na ubaya.

Kinywa cha mtu hunena yatokayo moyoni;

Suleimani anaandika juu ya shauri la mwanadamu na maisha yake, yaani maamuzi na maneno yanayotokana na mawazo ya mtu husika. Anasema mioyo ya watu imejaa hila, lakini anasisitiza shauri la Bwana kusimama. Suleiman anasema haja ya mwanadamu ni hisani yake, maana mwanadamu huwaza kutimiza haja zake, lakini anasisitiza kumcha Bwana akieleza kuwa heri maskini kuliko mwongo, maana mwongo hulenga kujinufaisha kwa njia zisizo sahihi.

Suleimani anahitimisha katika somo la leo kuwa kumcha Bwana kwa maskini humfanya kuuelekea uhai, maana hajiliwi na ubaya. Haimaanishi tuwe maskini, bali katika hali yoyote kumcha Bwana ndiko ndiyo kuwa hai. Mawazo yetu yawe mema kwa msaada wa Mungu ili maneno yetu yawe mema na yote tufanyayo yamshuhudie Kristo. Amina.

Ijumaa njema.

 

Heri Buberwa 

Mlutheri