MATANGAZO YA USHARIKA 

TAREHE 18 AGOSTI, 2024

SIKU YA BWANA YA 11 BAADA YA UTATU 

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI

NYENYEKEENI CHINI YA MKONO WA MUNGU 

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia kwa cheti. 

3. Matoleo ya Tarehe 11/08/2024

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 mchana. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV.

5. Kitenge chetu cha kiharaka kinapatikana hapo nje na kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya shilingi 40,000/= 

6. Wiki ijayo tarehe 25/08/2024 tutashiriki chakula cha Bwana. Washarika tujiandae.

7. Dayosisi ya Mashariki na Pwani inawataarifu kuwa kutakuwa na ratiba ya mitihani ya Shule ya Jumapili kama ifuatavyo:-

8. Tarehe 31/08/2024 Mtihani wa ufahamu ngazi ya Jimbo, saa 4.00 asubuhi Na tarehe 14/09/2024 Mtihani wa ufahamu ngazi ya Dayosisi saa 4.00 asubuhi .

9. Tarehe 06/10/2024 itakuwa ni sikukuu ya mavuno. Washarika tujiandae na kuiombea siku hiyo.

10. Shukrani: Jumapili ijayo tarehe 25/08/2024 katika ibada ya Kwanza saa 1.00 asubuhi, 

  • Familia ya Marehemu Mzee Hendry Adam Semali Lyatuu, watamshukuru Mungu kwa ulinzi wake tangu Baba yao alipougua na kuitwa Mbinguni tarehe. 5/6/2023 pamoja na kumponya Fredrick Allan Lyatuu.

 Neno: Zaburi 102:2-2, Wimbo: TMW 262, Kama si wewe (Kwaya ya Upendo)

  • Familia ya Dr na Bibi ONESMO itatoa Shukrani kwa Mjukuu weo GODWIN FREDRICK MWENDE Kupona tatizo la Figo.

Neno: 1 WAKORINTHO 15:10a, Wimbo: NI NEEMA (AGAPE KWAYA)

12. NDOA: NDOA ZA WASHARIKA 

KWA MARA YA PILI TUNATANGAZA NDOA YA TAREHE 31/08/2024

SAA 8.00 MCHANA

  • Bw. Martin John Lyanga na Bi. Martina Martin Mapujila 

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu.

13. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

  • Upanga: Kwa Bwana na Bibi Happiness Nkya
  • Mjini kati: Kwa Mama Omega Mongi
  • Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Bwana na Bibi Dan Mtunga
  • Kinondoni: Kwa Prof na Bibi Saitiel Kulaba
  • Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bwana na Bibi Francis Mwaitembo
  • Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach: Kwa Mama Elly Swai
  • Ilala, Chang’ombe, Buguruni: Kwa Bwana na Bibi James 
  • Oysterbay, Masaki: Kwa Mama Vicktoria Katikaza

14. Zamu: Zamu za wazee ni kundi la Kwanza 

Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.