Date: 
16-08-2024
Reading: 
Isaya 31:1-9

Ijumaa asubuhi tarehe 16.08.2024

Isaya 31:1-9

1 Ole wao watelemkao kwenda Misri wapate msaada, na kutegemea farasi; watumainio magari kwa kuwa ni mengi, na wapanda farasi kwa kuwa ni hodari sana; lakini hawamwangalii Mtakatifu wa Israeli, wala hawamtafuti Bwana!

2 Lakini yeye naye ana akili, naye ataleta uovu, wala hatayatangua maneno yake; bali ataondoka juu ya nyumba yao watendao mabaya, na juu ya msaada wa hao watendao maovu.

3 Basi Wamisri ni wanadamu wala si Mungu, na farasi zao ni nyama wala si roho; na Bwana atakaponyosha mkono wake, yeye asaidiaye atajikwaa, na yeye asaidiwaye ataanguka, nao wote pamoja watakoma.

4 Maana Bwana aniambia hivi, Kama vile ilivyo simba angurumapo na mwana-simba juu ya mawindo yake, wachungaji wengi wakiitwa ili kumpiga, lakini hatiwi hofu na sauti zao, wala kufanya woga kwa sababu ya mshindo wao; ndivyo Bwana wa majeshi atakavyoshuka ili kufanya vita juu ya mlima Sayuni, na juu ya kilima chake.

5 Kama ndege warukao, Bwana wa majeshi ataulinda Yerusalemu; ataulinda na kuuokoa, atapita juu yake na kuuhifadhi.

6 Mwelekeeni yeye mliyemwasi sana, enyi wana wa Israeli.

7 Maana katika siku hiyo kila mtu atatupa sanamu zake za fedha, na sanamu zake za dhahabu, ambazo mikono yenu imezifanya, zikawa dhambi kwenu.

8 Ndipo huyo Mwashuri ataanguka kwa upanga ambao si wa mtu; na upanga usio upanga wa mtu utamla; naye ataukimbia upanga, na vijana wake watatoa kodi.

9 Na mwamba wake utatoweka kwa sababu ya hofu, nao wakuu wake wataionea bendera hofu kuu, asema Bwana, ambaye moto wake u katika Sayuni, na tanuru yake katika Yerusalemu.

Mtafuteni Bwana nanyi mtaishi;

Ujumbe huu tunaousoma asubuhi ya leo, ulipelekwa kwa Israel na Nabii Isaya wakiwa bado hawajawa mateka kule Babeli. Isaya anawapa ujumbe wa kumwelekea Bwana waliyekuwa wamemuasi sana. Walikuwa wamemuasi Bwana maana kazi ya mikono yao zilikuwa dhambi, Isaya anasema wangezitupa katika siku ya hukumu. Ujumbe unawaambia kuelekea kuvamiwa (8) na Ashuru, lakini katika yote wanasisitizwa kumcha Bwana.

Kama tulivyoona, ujumbe wa Isaya ulihusu kumwelekea Bwana ambaye Israel walikuwa wamemuasi sana. Ujumbe huu unatukumbusha kumtafuta Bwana kwa kutubu dhambi zetu daima, maana tunayo ahadi ya kusamehewa dhambi. Somo limetoa "Ole" kwa wale ambao hawamtafuti Bwana, watendao maovu. Tuipuke hiyo "Ole" kwa kuishi maisha ya toba, msamaha na imani ya kweli ili tuishi katika Bwana, sasa na siku zote. Amina

Ijumaa njema

Heri Buberwa