MATANGAZO YA USHARIKA 

TAREHE 11 AGOSTI, 2024

SIKU YA BWANA YA 11 BAADA YA UTATU 

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI

MTAFUTENI BWANA NANYI MTAISHI 

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia kwa cheti. 

3. Matoleo ya Tarehe 04/08/2024

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 mchana. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV.

5. Kitenge chetu cha kiharaka kinapatikana hapo nje na kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya shilingi 40,000/= 

6. Leo tumepokea wageni wanakwaya kutoka dayosisi ya ziwa victoria Usharika wa Imani Kanisa Kuu, Kwaya ya Agape. Walifika ijumaa tarehe 09/08/2024. Wageni karibuni sana.

7. Dayosisi ya Mashariki na Pwani inawataarifu kuwa kutakuwa na ratiba ya mitihani ya Shule ya Jumapili kama ifuatavyo:-

8. Jumamosi ijayo tarehe 17/08/2024 kutakuwa na mtihani wa kupima ufahamu wa wanafunzi saa 4.00 asubuhi.

  • Tarehe 31/08/2024 Mtihani wa ufahamu ngazi ya Jimbo, saa 4.00 asubuhi
  • Na tarehe 14/09/2024 Mtihani wa ufahamu wa Jimbo ngazi ya Dayosisi saa 4.00 asubuhi .

 9. Tarehe 28/09/2024 na 29/09/2024 itakuwa ni sikukuu ya mikaeli na watoto. Hivyo tunaomba vikundi vyote vizingatie sherehe hii muhimu ili tuweze kuwaenzi, kuwatunza na kuwatia moyo watoto wetu kwa kuwachangia chochote ili kufanikisha Sikukuu hii. Mungu awabariki.

10. NDOA: NDOA ZA WASHARIKA 

KWA MARA YA KWANZA TUNATANGAZA NDOA YA TAREHE 31/08/2024

SAA 8.00 MCHANA

  • Bw. Martin John Lyanga na Bi. Martina Martin Mapujila

KWA MARA YA TATU TUNATANGAZA NDOA YA TAREHE 17/08/2024

SAA 9.00 ALASIRI

  • Bw. Solomon Elisa Msuya na Bi. Neema Selemani Shemngwa 

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu.

11. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

  • Upanga: Kwa Bwana na Bibi George Kinyaha
  • Mjini kati: Kwa Bwana na Bibi Lwaga
  • Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Bw na Bibi Charles Lyimo
  • Kinondoni: Kwa Bwana na Bibi Danford Mariki
  • Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bwana na Bibi Albert Olotu
  • Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach: Kwa Dr na Bibi Rumishaeli Shoo
  • Ilala, Chang’ombe, Buguruni: Kwa …………………………….
  • Oysterbay, Masaki: Kwa Bwana na Bibi Kimweri

14. Zamu: Zamu za wazee ni kundi la Pili 

Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.