Date: 
12-08-2024
Reading: 
Sefania 2:1-3

Jumatatu asubuhi tarehe 12.08.2024

Sefania 2:1-3

1 Jikusanyeni, naam, jikusanyeni, Ee taifa lisilo na haya;

2 kabla haijazaa hiyo amri, kabla haijapita siku ile kama makapi, kabla haijawajilia hasira kali ya Bwana, kabla haijawajilia siku ya hasira ya Bwana.

3 Mtafuteni Bwana, enyi nyote mlio wanyenyekevu wa dunia, ninyi mliozitenda hukumu zake; itafuteni haki, utafuteni unyenyekevu; huenda mtafichwa katika siku ya hasira ya Bwana.

Mtafuteni Bwana nanyi mtaishi;

Ujumbe wa Sefania ni hukumu ya Bwana ijayo. Sefania alileta ujumbe kwa Taifa la Mungu kuhusu hukumu, ujumbe ambao unaanzia sura ya kwanza;

Sefania 1:2

Nitavikomesha kabisa vitu vyote, visionekane juu ya uso wa nchi, asema Bwana.

Sefania anaendelea kuwapa ujumbe watu kumtafuta Bwana ili kuiepuka hukumu. Anawasisitiza kuitafuta haki, unyenyekevu ili kuiepuka hasira ya Bwana.

Sefania anapotoa ujumbe wa kumtafuta Bwana anawataka watu kuishi kwa kumcha Bwana, na kuitafuta haki ya Mungu. Ujumbe huo ndiyo tunaopewa asubuhi hii, kwamba tumtafute Bwana, tuwe wanyenyekevu ili kuiepuka hasira ya Bwana. Tuishi kwa njia ya neno la Kristo ili tuwe na mwisho mwema. Amina

Uwe na wiki njema 

Heri Buberwa