MATANGAZO YA USHARIKA
TAREHE 28 JULAI, 2024
SIKU YA BWANA YA 9 BAADA YA UTATU
NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI
MUNGU HUPENDEZWA NA MWENYE MOYO WA TOBA
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia kwa cheti. ili tuwakaribishe.
3. Matoleo ya Tarehe 21/07/2024
4. Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.
NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:
0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT
Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL
4. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 mchana. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV.
5. Kitenge chetu cha kiharaka kinapatikana hapo nje na kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya shilingi 40,000/=
6. Leo 28/07/2024 tutashiriki Chakula cha Bwana. Washarika karibuni.
7. Jumapili ijayo tarehe 04/08/2024 tutamtolea Mungu fungu la kumi. Washarika tujiandae.
8. Uongozi wa Umoja wa Wanawake unapenda kuwashukuru sana Wanawake waliohudhuria tamasha la uimbaji lililofanyika jana jumamosi tarehe 27/07/2024 Usharika wa Tabata. Mungu awabariki sana.
9. Usharika utapokea wageni wanakwaya kutoka dayosisi ya ziwa victoria Usharika wa Imani Kwaya ya Agape. Watafika siku ya ijumaa tarehe 09/08/2024. Wataondoka tarehe 12/08/2024 saa kumi jioni kuelekea mwanza. Watapokelewa na wenyeji wao kwaya ya Agape Azania front. Washarika tuendelee kuwaombea.
10. Ofisi kuu ya Vijana Jimbo la Kati, kwa kushirikiana na Mkuu wa Jimbo Mchg. Frank Kimambo wameandaa Kongamano la Vijana litakalofanyika katika Chuo cha Uhasibu Arusha tarehe 10 Septemba 2024 mpaka tarehe 15 Septemba 2024. Aidha, Dawati la Vijana Makao Makuu Arusha limeandaa Kongamano la Viongozi wa Vijana wa Sharika na Mitaa litakalofanyika Dodoma tarehe 4 Septemba 2024 mpaka tarehe 9 Septemba 2024. Gharama ya mshiriki mmoja kwa Makongamano yote Arusha na Dodoma ni TZS 300,000.00. Jimbo na Dayosisi wamewapa vijana fomu kwa ajili ya kuchangisha kwa washarika. Kwa moyo mkunjufu, Uongozi wa Umoja wa Vijana unaomba washarika kuwaunga mkono katika kukamilisha gharama hizi na kuwawezesha kuhudhuria.
11. SHUKRANI: Jumapili ijayo tarehe 04/08/2024 katika ibada ya kwanza. Familia ya Marehemu Elinsa Elimringi Nyange, inapenda kutoa sadaka ya kumshukuru Mungu kwa matendo makuu aliyowatendea.
Neno: Zaburi 34:1-4, Wimbo: TMW 273 (Kumtegemea Mwokozi).
12. NDOA: NDOA ZA WASHARIKA
KWA MARA YA KWANZA TUNATANGAZA NDOA YA TAREHE 17/08/2024
SAA 9.00 ALASIRI
-
Bw. Solomon Elisa Msuya na Bi. Neema Selemani Shemngwa
Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu.
13. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA
- Upanga: Kwa Bwana na bibi S. Nkya
- Mjini kati: Kwa Bwana na Bibi Dalali
- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Bwana na Bibi Charles Lyimo
- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Dr. na Bibi Ruhago
- Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach: Kwa Bwana na Bibi Elisha Mushumbusi .
14. Zamu: Zamu za wazee ni kundi la Pili
Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.