Date: 
20-07-2024
Reading: 
2 Timotheo 1:15-18

Jumamosi asubuhi tarehe 20.07.2024

2 Timotheo 1:15-18

15 Waijua habari hii, ya kuwa wote walio wa Asia waliniepuka, ambao miongoni mwao wamo Figelo na Hermogene.

16 Bwana awape rehema wale walio wa mlango wake Onesiforo; maana mara nyingi aliniburudisha, wala hakuuonea haya mnyororo wangu;

17 bali, alipokuwapo hapa Rumi, alinitafuta kwa bidii akanipata.

18 Bwana na ampe kuona rehema machoni pa Bwana siku ile. Na jinsi alivyonihudumia kwa mengi huko Efeso, wewe unajua sana.

Wito wa kuwajali wengine katika Kristo;

Mtume Paulo anamuandikia Timotheo juu ya ahadi ya uzima katika Kristo. Anamtaka Timotheo kuifundisha ahadi hii ya Kristo pasipo woga, na kuvumilia katika kazi hiyo ya Injili ili watu wote wamgeukie Kristo. 

Mtume Paulo anakazia kwa Timotheo kumhubiri Kristo aliyeuokoa Ulimwengu kwa neema;

2 Timotheo 1:9-10

9 ambaye alituokoa akatuita kwa mwito mtakatifu, si kwa kadiri ya matendo yetu sisi, bali kwa kadiri ya makusudi yake yeye na neema yake. Neema hiyo tulipewa katika Kristo Yesu tangu milele,

10 na sasa inadhihirishwa kwa kufunuliwa kwake Mwokozi wetu Kristo Yesu; aliyebatili mauti, na kuufunua uzima na kutokuharibika, kwa ile Injili;

Ni katika kumalizia ujumbe huo, tunaona katika somo Paulo akiwakumbuka waliomhudumia katika kazi ya Injili huko Efeso, na hata Rumi. Mchango wao ulikuwa muhimu sana kwa Paulo katika Injili ndiyo maana aliwakumbuka katika waraka. Kuwajali wengine katika maisha yetu hutuweka pamoja kama kundi la Mungu. Utume mwema. 

Jumamosi njema.

 

Heri Buberwa