Date: 
13-07-2024
Reading: 
Mithali 6:6-12

Jumamosi asubuhi tarehe 13.07.2024

Mithali 6:6-11

6 Ewe mvivu, mwendee chungu, Zitafakari njia zake ukapate hekima.

7 Kwa maana yeye hana akida, Wala msimamizi, wala mkuu,

8 Lakini hujiwekea akiba ya chakula wakati wa jua; Hukusanya chakula chake wakati wa mavuno.

9 Ewe mvivu, utalala hata lini? Utaondoka lini katika usingizi wako?

10 Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo, Bado kukunja mikono upate usingizi!

11 Hivyo umaskini wako huja kama mnyang'anyi, Na uhitaji wako kama mtu mwenye silaha.

Bidii ya kijana, mafanikio ya Kanisa;

Jumapili iliyopita katika Homilia Takatifu nilirejea pia somo hilo hapo tulilosoma, nilipokuwa nakazia kwamba uvivu huleta umaskini. Mwandishi anatoa mfano wa chungu ambaye ni mdudu mdogo, kwamba hufanya kazi bila usimamizi na hujiwekea akiba ya chakula cha kutosha wakati wote. Mwandishi anaelekeza kufanya kazi na kuacha uvivu kama alivyo chungu ili kuwa na mafanikio.

Changu afanyaye kazi bila usimamizi ni picha ya kujitambua, bidii, maarifa, juhudi na kufanya kazi bila kuchoka. Kufanya kazi ni ibada yenye utukufu maana uvivu ni dhambi. Kwa utume wa hakika hatuwezi kukwepa kufanya kazi. Fanya kazi kwa bidii kwa utukufu wa Mungu. Amina

Jumamosi njema 

Heri Buberwa