Date: 
08-07-2024
Reading: 
Mithali 8:17-18

Jumatatu asubuhi tarehe 08.07.2024

Mithali 8:17-18

17 Nawapenda wale wanipendao, Na wale wanitafutao kwa bidii wataniona.

18 Utajiri na heshima ziko kwangu, Naam, utajiri udumuo, na haki pia.

Bidii ya kijana, mafanikio ya Kanisa;

Asubuhi hii tunasoma juu ya Bwana kuwapenda wampendao, na wote wamtafutao kwa bidii kumuona. Hapa inaelezwa kwamba Bwana huwapokea wote wamwaminio, na kuwatunza daima wakaapo kwake. Bwana anasema utajiri na heshima uko kwake, yaani bidii katika Bwana huleta mafanikio. 

Ujumbe wa asubuhi ya leo ni kumpenda Bwana, yaani kudumu katika imani siku zote tukiwa na bidii katika kutimiza wajibu wetu kuelekea mafanikio. Kumpenda Bwana ni kumwamini, kulishika neno lake, kumfuata na kutenda yapasayo. Tukifanya hayo na kufanya kazi kwa bidii tunafanikiwa, na ufalme wa Mungu unadhihirika pote. Tumshike Bwana na kufanya kazi kwa bidii ili kazi ya Bwana isonge mbele. Amina.

Uwe na wiki njema 

Heri Buberwa