Date: 
11-06-2024
Reading: 
Eziekeli 44:1-9

Jumanne asubuhi tarehe 11.06.2024

Ezekieli 44:1-9

1 Kisha akanirudisha kwa njia ya lango lile la nje, la mahali patakatifu lililoelekea upande wa mashariki; nalo lilikuwa limefungwa.

2 Bwana akaniambia, Lango hili litafungwa, halitafunguliwa, wala mtu awaye yote hataingia kwa lango hili, kwa maana Bwana, Mungu wa Israeli, ameingia kwa hilo; basi kwa sababu hiyo litafungwa.

3 Na mkuu, yeye ndiye atakayeketi ndani yake ale chakula mbele za Bwana; ataingia kwa njia ya ukumbi wa lango, naye atatoka kwa njia iyo hiyo.

4 Kisha akanileta, kwa njia ya lango la upande wa kaskazini, mbele ya nyumba; nikaangalia, na tazama, huo utukufu wa Bwana uliijaza nyumba ya Bwana; nikaanguka kifudifudi.

5 Bwana akaniambia, Mwanadamu, weka moyoni mwako, ukatazame kwa macho yako, ukasikie kwa masikio yako, maneno yote nitakayokuambia, katika habari ya kawaida zote za nyumba ya Bwana, na ya amri zake zote; nawe weka moyoni mwako maingilio ya nyumba, pamoja na matokeo yote ya mahali patakatifu.

6 Nawe utawaambia waasi, yaani nyumba ya Israeli, Bwana MUNGU asema hivi; Enyi nyumba ya Israeli, katika machukizo yenu yote, na iwatoshe,

7 kuwa mmewaingiza wageni, ambao mioyo yao haikutahiriwa, wala miili yao haikutahiriwa, wawe ndani ya patakatifu pangu, wapatie unajisi, naam, nyumba yangu, mtoapo sadaka ya chakula changu, mafuta na damu; nao wameyavunja maagano yangu, juu ya machukizo yenu yote.

8 Wala hamkuvilinda vitu vyangu vitakatifu bali mmejiwekea walinzi wa kawaida zangu, katika patakatifu pangu.

9 Bwana MUNGU asema hivi; Hapana mgeni, ambaye moyo wake haukutahiriwa, wala mwili wake haukutahiriwa, atakayeingia patakatifu pangu, miongoni mwa wageni walio kati ya wana wa Israeli.

Heri wenye moyo safi;

Sura ya 44 ni ujumbe wa Yeremia kwa Wayahudi waliokuwa Misri juu ya ibada yao ya sanamu. Mistari tisa tuliyosoma ni utangulizi wa uovu wao wa ibada ya sanamu, na Bwana anasema kwa uovu wao hawatamkaribia. Kumbe tunaona kwamba Mungu alichukia kwa watu wake kuabudu miungu, badala ya kumcha yeye.

Ukisoma mbele unaona ujumbe wa Bwana kwa wale Wayahudi ambao hawakumcha;

Ezekieli 44:12-13

12 Kwa sababu waliwahudumia mbele ya vinyago vyao, wakawa kwazo la uovu kwa nyumba ya Israeli; basi nimeuinua mkono wangu juu yao, asema Bwana MUNGU, nao watachukua uovu wao.
13 Wala hawatanikaribia, kunihudumia katika kazi ya ukuhani, wala hawatakaribia vitu vyangu vitakatifu kimojawapo, vitu vilivyo vitakatifu sana; bali watachukua aibu yao, na machukizo yao yote waliyoyatenda.

Hadi hapa tunaweza kuona kuwa ujumbe wa Bwana uliwalenga watu ambao waliabudu miungu, hawakumwabudu yeye. Hawakuwa na moyo safi kwa sababu ya ibada ya sanamu. Tumtangulize Bwana katika mambo yote, hiyo ndiyo ibada njema mbele za Bwana. Amina.

Jumanne njema 

 

Heri Buberwa