Date: 
01-06-2024
Reading: 
1 Wathesalonike 4:9-12

Jumamosi asubuhi tarehe 01.06.2024

1 Wathesalonike 4:9-12

9 Katika habari ya upendano, hamna haja niwaandikie; maana ninyi wenyewe mmefundishwa na Mungu kupendana.

10 Kwa maana mnafanya neno hili kwa ndugu wote walio katika Makedonia yote. Lakini twawasihi, ndugu, mzidi sana.

11 Tena mjitahidi kutulia, na kutenda shughuli zenu, na kufanya kazi kwa mikono yenu wenyewe, kama tulivyowaagiza;

12 ili mwenende kwa adabu mbele yao walio nje, wala msiwe na haja ya kitu cho chote.

Utatu Mtakatifu; Iweni na nia ya Kristo;

Mtume Paulo anawakumbusha Wathesalonike juu ya fundisho la zamani kabisa linalohusu upendo. Anawaambia kwamba walifundishwa kupendana toka zamani, akiwataka kuendeleza upendo huo kwa ndugu wote. Anawasisitiza kufanya kazi zao kwa upendo, ushirikiano na umoja, ili kulijenga Kanisa la Mungu.

Hata sisi tumefundishwa upendo toka zamani. Tunasoma kwenye maandiko, toka Agano la kale jinsi Mungu alivyoupenda ulimwengu akamuumba mwanadamu kwa mfano wake. Amri za Mungu pia ni huashiria upendo kamili. Kwa amri hizo hizo, Yesu Kristo alifundisha kuwa amri kuu ni upendo. Hivyo, msingi wa umoja wetu ni upendo. Tupendane. Amina. 

Ijumaa njema.

 

Heri Buberwa 

Mlutheri