Date: 
30-05-2024
Reading: 
1Wakorintho 12:28-31

Alhamisi asubuhi tarehe 30.05.2024

1 Wakorintho 12:28-31

28 Na Mungu ameweka wengine katika Kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii, wa tatu waalimu, kisha miujiza, kisha karama za kuponya wagonjwa, na masaidiano, na maongozi, na aina za lugha.

29 Je! Wote ni mitume? Wote ni manabii? Wote ni waalimu? Wote wanatenda miujiza?

30 Wote wana karama za kuponya wagonjwa? Wote wanena kwa lugha? Wote wafasiri?

31 Takeni sana karama zilizo kuu. Hata hivyo nawaonyesha njia iliyo bora.

Utatu Mtakatifu; Iweni na nia ya Kristo;

Mtume Paulo anaendelea kufundisha juu ya umoja wa Kanisa anapoonesha umuhimu wa ushirika miongoni mwa waaminio. Paulo anaandika kwamba ushirika ni muhimu miongoni mwa mitume, manabii, walimu na wote wenye karama mbalimbali. Hawa wakifanya kazi kwa pamoja huduma ya Kanisa inawafikia wengi kwa urahisi, maana vipawa tofauti vinaungana kuhubiri.

Kwa leo naweza kusema huduma zote ni muhimu kufanya kazi kwa pamoja kuanzia kwa Wachungaji, Wainjilisti, Wazee wa Kanisa, Waimbaji, Wafanya usafi, Wapiga kengele, Madreva, Walimu wa shule ya Jumapili, Wahasibu, makarani na wengineo wote.

Tuwe na umoja, tukihudumu kwa pamoja kwa ajili ya Utukufu wa Mungu. Amina.

Alhamisi njema 

Heri Buberwa