Date: 
28-05-2024
Reading: 
1Wakorintho 12:12-17

Jumanne asubuhi tarehe 28.05.2024

1 Wakorintho 12:12-27

12 Maana kama vile mwili ni mmoja, nao una viungo vingi, na viungo vyote vya mwili ule, navyo ni vingi, ni mwili mmoja; vivyo hivyo na Kristo.

13 Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu Wayahudi, au kwamba tu Wayunani; ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru; nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja.

14 Kwa maana mwili si kiungo kimoja, bali ni vingi.

15 Mguu ukisema, Kwa kuwa mimi si mkono, mimi si wa mwili; je! Si wa mwili kwa sababu hiyo?

16 Na sikio likisema, Kwa kuwa mimi si jicho, mimi si la mwili; je! Si la mwili kwa sababu hiyo?

17 Kama mwili wote ukiwa jicho, ku wapi kusikia? Kama wote ni sikio ku wapi kunusa?

18 Bali Mungu amevitia viungo kila kimoja katika mwili kama alivyotaka.

19 Lakini kama vyote vingekuwa kiungo kimoja, mwili ungekuwa wapi?

20 Lakini sasa viungo ni vingi, ila mwili ni mmoja.

21 Na jicho haliwezi kuuambia mkono, Sina haja na wewe; wala tena kichwa hakiwezi kuiambia miguu, Sina haja na ninyi.

22 Bali zaidi sana vile viungo vya mwili vidhaniwavyo kuwa vinyonge zaidi vyahitajiwa zaidi.

23 Na vile viungo vya mwili vidhaniwavyo kuwa havina heshima, viungo vile twavipa heshima zaidi; na viungo vyetu visivyo na uzuri vina uzuri zaidi sana.

24 Kwa maana viungo vyetu vilivyo na uzuri havina uhitaji; bali Mungu ameuungamanisha mwili, na kukipa heshima zaidi kile kiungo kilichopungukiwa;

25 ili kusiwe na faraka katika mwili, bali viungo vitunzane kila kiungo na mwenziwe.

26 Na kiungo kimoja kikiumia, viungo vyote huumia nacho, na kiungo kimoja kikitukuzwa, viungo vyote hufurahi pamoja nacho.

27 Basi ninyi mmekuwa mwili wa Kristo, na viungo kila kimoja peke yake.

Utatu Mtakatifu; Iweni na nia ya Kristo;

Somo linahusu mwili wa Kristo. Katika kujadili hili, Mtume Paulo anawaandikia Wakorintho mfano wa viungo vya mwili, kwamba viko tofauti tofauti lakini vinafanya kazi pamoja kwenye mwili mmoja ule ule. Sikio, jicho, mkono, mguu, ulimi, vidole na viungo vingine vyote viko katika mwili mmoja.

Paulo ndipo anakuja na fundisho kuwa sisi tu viungo vya mwili wa Kristo. Yaani viungo ni vingi, lakini mwili ni mmoja. Kumbe kila mmoja akitumia karama yake katika utume wetu, kazi ya Mungu itafanyika ipasavyo. Maana yake tuwe na umoja katika Bwana ili kulitangaza jina lake. Amina.

Jumanne njema.

Heri Buberwa