Date: 
18-05-2024
Reading: 
Daniel 9:20-23

Jumamosi asubuhi 18.05.2024

Danieli 9:20-23

20 Basi hapo nilipokuwa nikisema, na kuomba, na kuiungama dhambi yangu, na dhambi ya watu wangu Israeli, na kuomba dua yangu mbele za Bwana, Mungu wangu, kwa ajili ya mlima mtakatifu wa Mungu wangu;

21 naam, nilipokuwa nikinena katika kuomba, mtu yule, Gabrieli, niliyemwona katika njozi hapo kwanza, akirushwa upesi, alinigusa panapo wakati wa dhabihu ya jioni.

22 Akaniagiza, akaongea nami, akasema, Ee Danielii, nimetokea sasa, ili nikupe akili upate kufahamu.

23 Mwanzo wa maombi yako ilitolewa amri, nami nimekuja kukupasha habari; maana wewe unapendwa sana; basi itafakari habari hii, na kuyafahamu maono haya.

Omba! Mungu anasikia kuomba kwetu;

Nabii Danieli alifanya toba kwa ajili ya Taifa la Mungu. Ni baada ya wana wa Israeli kutowasikiliza manabii wa Mungu na kutenda kinyume na maagizo waliyopewa na manabii. Tunaweza kusoma kwa sehemu jinsi Danieli alivyofanya sala ya toba;

Sehemu ya sala ya toba;

Danieli 9:5-6, 9-10

5 tumefanya dhambi, tumefanya ukaidi, tumetenda maovu, tumeasi, naam, hata kwa kuyaacha maagizo yako na hukumu zako;
6 wala hatukuwasikiliza watumishi wako, manabii, ambao kwa jina lako walisema na wafalme wetu, na wakuu wetu, na baba zetu, na watu wote wa nchi.
9 Rehema na msamaha ni kwa Bwana Mungu wetu, ingawa tumemwasi;
10 wala hatukuitii sauti ya Bwana, Mungu wetu, kwa kwenda katika sheria zake, alizoziweka mbele yetu kwa kinywa cha watumishi wake, manabii.

Somo linaonesha toba kukubaliwa na Bwana kwa njia ya malaika wa Bwana (21). Mstari wa 23 pia unaonesha upendo wa Mungu asikiaye maombi ya watu wake. Nasi tunakumbushwa kuomba kwa jina la Yesu atupendaye, ambaye husikia maombi yetu. Amina.

Jumamosi njema

Heri Buberwa