Date: 
16-05-2024
Reading: 
Isaya 62:1-9

Alhamisi asubuhi tarehe 16.05.2024

Isaya 62:6-9

6 Nimeweka walinzi juu ya kuta zako, Ee Yerusalemu; hawatanyamaza mchana wala usiku; ninyi wenye kumkumbusha Bwana, msiwe na kimya;

7 wala msimwache akae kimya, mpaka atakapoufanya imara Yerusalemu, na kuufanya kuwa sifa duniani.

8 Bwana ameapa kwa mkono wake wa kuume, na kwa mkono wa nguvu zake, Hakika sitawapa adui zako nafaka yako tena kuwa chakula chao; wala wageni hawatakunywa divai yako, uliyoifanyia kazi.

9 Lakini walioivuna, ndio watakaoila, na kumhimidi Bwana; na walioichuma, ndio watakaoinywa, ndani ya nyua za patakatifu pangu.

Omba! Mungu anasikia kuomba kwetu;

Mungu kupitia kwa Nabii Isaya anaahidi kuilinda Yerusalemu. Bwana alikuwa amewarejesha wana wa Israeli kutoka uhamishoni, akawa anawapa hakikisho la kuwa nao daima. Haishii kuahidi kuwalinda, bali anawatangazia wokovu ikiwa watamcha yeye Mungu, aliyewakomboa.

Yapo mafundisho yanayosema Bwana aliahidi kuilinda Yerusalemu ya sasa iliyoko Mashariki ya kati kule Israeli. 

Baada ya Kristo kufa na kufufuka, tafsiri ya mji wa Yerusalemu ni wote waliompokea na kumwamini Yesu kama Mwokozi wao. Yesu huyu ndiye hutuita kumuomba kwa imani maana yeye husikia maombi yetu. Amina.

Alhamisi njema.

 

Heri Buberwa