Date: 
10-05-2024
Reading: 
Matendo ya Mitume 1:6-11

Ijumaa asubuhi tarehe 10.05.2024

Matendo ya Mitume 1:6-11

6 Basi walipokutanika, wakamwuliza, wakisema, Je! Bwana, wakati huu ndipo unapowarudishia Israeli ufalme?

7 Akawaambia, Si kazi yenu kujua nyakati wala majira, Baba aliyoyaweka katika mamlaka yake mwenyewe.

8 Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.

9 Akiisha kusema hayo, walipokuwa wakitazama, akainuliwa, wingu likampokea kutoka machoni pao.

10 Walipokuwa wakikaza macho mbinguni, yeye alipokuwa akienda zake, tazama, watu wawili wakasimama karibu nao, wenye nguo nyeupe,

11 wakasema, Enyi watu wa Galilaya, mbona mmesimama mkitazama mbinguni? Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni.

Kristo amepaa katika Utukufu wake;

Baada ya Yesu kufufuka, alipaa mbinguni baada ya siku 40, akirudi kwa Baba yake. Ni baada ya kazi yake hapa duniani, kama Mungu kweli na mwanadamu kweli. 

Kupaa kwa Yesu kuliashiria nini?

1. Kupaa kwa Yesu kuliashiria kazi yake hapa duniani kumalizika.

2. Kupaa kwa Yesu kuliashiria kuendelea kwa kazi yake, akiwa mbinguni.

3. Kupaa kwa Yesu kuliashiria mwanzo wa sisi kufanya utume wake kama alivyotutuma.

Sasa basi, Yesu alipaa kwenda mbinguni baada ya kufufuka kama tulivyoona. Bado anaendelea kutenda kazi yake kwa wote waaminio. Tuendelee kumwamini huyu Yesu aliyepaa, maana ndiye aliyekuwepo, yupo na ataendelea kuwepo, na mwisho ndiye atakayerudi kulichukua Kanisa lake.

Siku njema.

 

Heri Buberwa