Date: 
03-05-2024
Reading: 
Hesabu 21:16-20

Ijumaa asubuhi tarehe 03.05.2024

Hesabu 21:16-20

16 Kutoka huko wakasafiri kwenda Beeri; ni kisima ambacho Bwana alimwambia Musa, Uwakutanishe watu, nami nitawapa maji.

17 Ndipo Israeli wakaimba wimbo huu; Bubujika Ee kisima; kiimbieni;

18 Kisima walichokichimba wakuu, Ambacho wakuu wa watu wakakifukua, Kwa fimbo za enzi, kwa fimbo zao.

19 na kutoka Matana wakaenda Nahalieli; na kutoka Nahalieli wakaenda Bamothi;

20 na kutoka Bamothi wakaenda bondeni kwenye konde la Moabu, hata kilele cha Pisga, kielekeacho chini jangwani.

Njooni tumwimbie Bwana;

Safari ya wana wa Israeli kuelekea nchi ya ahadi inaendelea. Kuna wakati walimlalamikia Musa kwamba kwa nini aliwatoa Misri, maana sasa waliona wanataabika. Mungu alituma nyoka wakawauma wakafa kwa wingi. Baada ya toba, Musa alifanya nyoka wa shaba na kila aliyemtazama akaishi.

Ndipo wakaendelea na safari, Mungu akiendelea kuwa nao. Somo linaonesha Musa akiendelea kuwaongoza, Mungu akimuelekeza Musa kuwakutanisha ili awape maji. Hapa ndipo Israeli waliimba sifa kwa neema hii. Nasi tunaalikwa kumuimbia na kumsifu Bwana kwa neema ya wokovu. Amina.

Ijumaa njema 

 

Heri Buberwa