Date: 
01-05-2024
Reading: 
Luka 2:12-14

Jumatano asubuhi tarehe 01.05.2024

Luka 2:12-14

12 Na hii ndiyo ishara kwenu; mtamkuta mtoto mchanga amevikwa nguo za kitoto, amelala katika hori ya kulia ng'ombe.

13 Mara walikuwapo pamoja na huyo malaika, wingi wa jeshi la mbinguni, wakimsifu Mungu, na kusema,

14 Atukuzwe Mungu juu mbinguni, Na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia.

Njooni tumwimbie Bwana;

Wakati Yesu amezaliwa, wachungaji makondeni walikuwa wanachunga kondoo, utukufu wa Bwana ukawang'aria. Mara malaika aliwatokea wale wachungaji na kuwapa habari njema ya kuzaliwa kwa Mwokozi, Yesu Kristo.

Sasa ujumbe tuliousoma (soma tena) ni ujumbe wa malaika kwa wachungaji kuhusu mtoto Yesu. Ukisoma zaidi unaona malaika wakienda kumuona mtoto, halafu wanarudi wakimsifu Mungu. Nasi tunaalikwa kumsifu Mungu kwa ukombozi aliotupa, kwa kutenda yatupasayo. Amina 

 

Heri Buberwa