Date: 
20-04-2024
Reading: 
Mathayo 8:28-34

Jumamosi asubuhi tarehe 20.04.2024

Mathayo 8:28-34

28 Naye alipofika ng'ambo, katika nchi ya Wagerasi, watu wawili wenye pepo walikutana naye, wanatoka makaburini, wakali mno, hata mtu asiweze kuipitia njia ile.

29 Na tazama, wakapiga kelele, wakisema, Tuna nini nawe, Mwana wa Mungu? Je! Umekuja kututesa kabla ya muhula wetu?

30 Basi, kulikuwako mbali nao kundi la nguruwe wengi wakilisha.

31 Wale pepo wakamsihi, wakisema, Ukitutoa, tuache twende, tukaingie katika lile kundi la nguruwe.

32 Akawaambia, Nendeni. Wakatoka, wakaingia katika nguruwe; na kumbe! Kundi lote wakatelemka kwa kasi gengeni hata baharini, wakafa majini.

33 Lakini wachungaji walikimbia, wakaenda zao mjini, wakazieneza habari zote na habari za wale wenye pepo pia.

34 Na tazama, mji wote ukatoka kwenda kumlaki Yesu; nao walipomwona, walimsihi aondoke mipakani mwao.

Bwana huchunga na kulisha kundi lake;

Yesu anakutana na watu wawili wenye pepo wakitoka makaburini. Wawili hawa hawakuwa katika hali ya kawaida, kiasi ambacho mtu asingepita njia ile. Pepo walishindwa kuhimili nguvu ya Yesu Kristo, wakaomba wakaingie katika kundi la nguruwe. Nguruwe waliingiwa na pepo wakafa maji wote. Wachungaji wa nguruwe wakaenda mjini wakitangaza habari za Yesu.

Yesu anaonesha kujali kwake kwa kuwatoa wawili tuliowasoma pepo. Hakuwapita, hakuwaacha.

Yesu yuko vilevile, kwamba hutujali hata sasa. Hutualika kumfuata na kumtegemea daima, ili tuishi ndani yake na yeye ndani yetu kuelekea uzima wa milele. Amina.

Jumamosi njema 

Heri Buberwa