Date: 
16-04-2024
Reading: 
Hosea 14:4-8

Jumanne asubuhi tarehe 16.04.2024

Hosea 14:4-8

4 Mimi nitawaponya kurudi nyuma kwao; nitawapenda kwa ukunjufu wa moyo; kwa maana hasira yangu imemwacha.

5 Nitakuwa kama umande kwa Israeli; naye atachanua maua kama nyinyoro, na kuieneza mizizi yake kama Lebanoni.

6 Matawi yake yatatandaa, na uzuri wake utakuwa kama uzuri wa mzeituni, na harufu yake kama Lebanoni.

7 Na wao wakaao chini ya uvuli wake watarejea; watafufuka kama ngano, na kuchanua maua kama mzabibu; harufu yake itakuwa kama harufu ya divai ya Lebanoni.

8 Efraimu atasema, Mimi nina nini tena na sanamu? Mimi nimeitika, nami nitamwangalia. Mimi ni kama mberoshi wenye majani mabichi. Kwangu mimi yamepatikana matunda yako.

Bwana huchunga na kulisha kundi lake;

Hosea anamalizia unabii wake katika sura ya kumi na nne. Anaianza sura hii kwa kuwaita Israeli kumrudia Bwana. Anawaita kuacha maovu yote na kutenda yaliyo mema. Mstari wa nne ni hakikisho la Mungu kuwaponya na kuwasamehe Israeli kwa upendo. Israeli wanaitwa kwenda katika njia ya Bwana, maana njia za Bwana zimenyooka, yaani waache uovu.

Wito wa Bwana kwetu ni wa kudumu siku zote. Hutuita kumwamini na kumfuata siku zote za maisha yetu. Hivyo tunaalikwa kwenda katika njia ya Bwana, yaani kumwamini Yesu tukitenda yatupasayo. Tusiipuuze neema ya wito huu, ili tuurithi uzima wa milele. Amina.

Jumanne njema.

Heri Buberwa