Date: 
23-03-2024
Reading: 
Waebrania 7:23-25

Hii ni Kwaresma 

Jumamosi asubuhi tarehe 23.03.2024

Waebrania 7:23-25

23 Tena wale walifanywa makuhani wengi, kwa sababu wazuiliwa na mauti wasikae;

24 bali yeye, kwa kuwa akaa milele, anao ukuhani wake usioondoka.

25 Naye, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee.

Kwa Yesu kuna upatanisho wa kweli;

Somo la asubuhi ya leo linakuja baada ya kuona Makuhani wa kale walivyotenda kazi yao ya kuwaleta watu kwa Mungu. Lakini ukuhani huu ulikuja kubadilika baada ya Kristo kuja kama tunavyosoma;

Waebrania 7:12

Maana ukuhani ule ukibadilika, hapana budi sheria nayo ibadilike.

Kristo anatajwa kuwa Kuhani Mkuu kwa ajili ya wote waaminio. Yeye ndiye mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu. Tofauti yake na makuhani wa kale ni kwamba makuhani wale walichinja mnyama kupatanisha watu na Mungu, lakini Yesu alitupatanisha alipokufa msalabani na kufufuka. Tumwamini yeye daima. Amina.

Jumamosi njema.

Heri Buberwa