Date: 
22-03-2024
Reading: 
Marko 10:45

Hii ni Kwaresma 

Ijumaa asubuhi tarehe 22.03.2024

Marko 10:45

Kwa maana Mwana wa Adamu naye hakuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi.

Kwa Yesu kuna upatanisho wa kweli;

Yakobo na Yohana wakiwa na mama yao walimwendea Yesu wakiomba kukaa naye, mmoja akae kulia na mwingine kushoto. Yesu aliwaambia hawajui walichokuwa wakiomba, ila akawaambia habari ya kukaa kulia au kushoto kwake ni kwa ajili ya waliowekewa tayari.

Baada ya tukio hilo, wale wanafunzi wengine kumi walikasirika, maana waliona wenzao walitaka kukaa na Yesu wenyewe.

Mstari tuliousoma ni Yesu akiwatuliza wanafunzi, kwamba wadumu katika yeye (Yesu) aliyetoa nafsi yake iwe fidia ya wengi. Yaani aliwaambia wasiwazie tu kukaa na Yesu, bali wamwamini yeye aliye Mwokozi wa Ulimwengu kwa ajili ya uzima wa milele. Mwamini sasa uokolewe. Amina

Ijumaa njema.

 

Heri Buberwa