Date: 
21-03-2024
Reading: 
Luka 23:33-34

Hii ni Kwaresma 

Alhamisi asubuhi tarehe 21.03.2024

Luka 23:33-34

33 Na walipofika mahali paitwapo Fuvu la Kichwa, ndipo walipomsulibisha yeye, na wale wahalifu, mmoja upande wa kuume, na mmoja upande wa kushoto.

34 Yesu akasema, Baba, uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo. Wakagawa mavazi yake, wakipiga kura.

Kwa Yesu kuna upatanisho wa kweli;

Luka sura ya 23 inaandika Yesu akipelekwa mbele ya Pilato na kushtakiwa, Pilato anamuona bila kosa na kumpeleka kwa Herode. Herode naye anamdhihaki na kumrudisha kwa Pilato. Pilato alizidiwa na nguvu ya uuma, hata alipotaka kumuachia umma ukakataa. Ikabidi Yesu asulibiwe.

Ndipo katika somo tunaona Yesu akisulubishwa msalabani na wahalifu wawili, mmoja kulia na mwingine kushoto. Tunasoma Yesu akiwa msalabani, lakini anawaombea waliomsulibisha kwa Baba awasamehe.

Kwa njia ya mateso na kifo msalabani, alitupatanisha naye. Tudumu katika upatanisho huu tukitenda yatupasayo, leo na daima. Amina.

Alhamisi njema 

Heri Buberwa