MATANGAZO YA USHARIKA 

TAREHE 17 MACHI, 2024

SIKU YA BWANA YA 2 KABLA YA PASAKA

NENO LINALOTUONGOZA NI

KWA YESU KUNA UPATANISHO WA KWELI 

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna Mgeni aliyetufikia kwa cheti. 

3. Matoleo ya Tarehe 10/03/2024

4. Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 mchana. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV. 

6. Jumatano ijayo tarehe 28/03/2024 saa 11.00 jioni tutaendelea na ibada ya Kwaresma ambayo ndiyo itakuwa ya mwisho. Zamu za Wazee itakuwa ni kundi la pili. 

7. Jumamosi ijayo tarehe 23/03/2024 saa 3.00 asubuhi Wanawake wote Jimbo la kati watafanya ibada ya Maadhimisho ya pasaka. Maadhimisho hayo yatafanyika Kijimbo Usharika wa Kitunda Kuu. Wanawake wote mnaombwa kuhudhuria ibada hii.

8. Mazoezi ya umoja yataendelea siku ya jumanne saa 11:00 jioni kwa ajili ya Maandalizi ya Pasaka. Wanakwaya wote mnaombwa kuhudhuria na kufika kwa wakati.

9. Jumapili ijayo tarehe 24/03/2024 ni siku ya Mitende.

10. Jumamosi ijayo tarehe 23/03/2024 kutakuwa na Ibada ya Wazee kuanzia miaka 60 na kuendelea. Ibada itafanyika hapa usharikani Azania Front Cathedral kuanzia saa 3.00 asubuhi ambayo itaambatana na Chakula cha Bwana. Wazee wote wanakaribishwa sana.

11. KIPINDI CHA MWISHO CHA MAFUNDISHO MAALUM YA MSIMU WA KWARESMA 2024 kitaendelea siku ya Ahamisi na Ijumaa, kuanzia saa 11:00 jioni, tutakuwa na Mafundisho, Maombi na Maombezi. Kichwa cha mafundisho hayo ni 

" NIA YA UPENDO WA KRISTO KWA FAMILIA " Neno la kusimamia ni kutoka Yoe‬l 2:12-‬14‬ ‬‬‬‬‬‬‬‬ Wote mnakaribishwa."‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬

12. SHUKRANI: Jumapili ijayo 24/03/2024 katika ibada ya Tatu saa 4.30 asubuhi 

  • Famili ya Marehemu Mzee Philemon Mgaya watatoa shukrani kwa kuwatia nguvu toka Mama yao mpendwa Anna Philemon Mgaya ambaye aliwahi kuwa Mzee wa kanisa hapa Azania Front alipotwaliwa na Bwana miaka 20 iliyopita pamoja na wanafamilia wengine ambao pia waliitwa na Bwana, Baba mzazi Mzee Philemon Mgaya, Dada Lillian Mgaya na Kaka Eric Mgaya. Mungu aendelee kuwapa pumziko la amani.

Neno: Zaburi ya 118:1, Wimbo: TMW 262 Tumshukuru Mungu

13. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

  • Upanga: Watatangaziana
  • Mjini kati: Watatangaziana
  • Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Mama Mamkwe.
  • Kinondoni: Kwa Bwana na Bibi Danford Mariki
  • Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Dr. Abedi na Eng. Elisifa Kinasha
  • Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach: Ilala, Chang’ombe, Buguruni: Oysterbay, Masaki: Watashiriki ibada za jumatano hapa Kanisani

14. Zamu: Zamu za wazee ni kundi la Kwanza.

Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.