Date: 
27-01-2024
Reading: 
Efeso 1:11-12

Jumamosi tarehe 27/11/2024 Asubuhi 

Efeso 1:11-12

11 na ndani yake sisi nasi tulifanywa urithi, huku tukichaguliwa tangu awali sawasawa na kusudi lake yeye, ambaye hufanya mambo yote kwa shauri la mapenzi yake.

12 Nasi katika huyo tupate kuwa sifa ya utukufu wake, sisi tuliotangulia kumwekea Kristo tumaini letu

Mungu hubariki familia zetu

Katika neno la leo tunaona kuwa Kristo alituchagua tangu awali kuwa watu wake ili tupate kuwa sifa ya utukufu wake. Hivyo tunapaswa kumweka Kristo kuwa tumaini letu ili aweze kudumu ndani yetu.

Siku njema.