Event Date: 
31-12-2023

Washarika wa Azania Front walijumuika siku ya Jumapili tarehe 31/12/2023, siku ya mwisho kabisa ya mwaka 2023 ili kumshukuru Mungu kwa matendo makubwa aliyowafanyia.

Katika ibada hiyo iliyoongozwa na Msaidizi wa Baba Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Dean Chediel Lwiza akisaidiwa na Mchungaji Kiongozi wa Usharika, Chaplain Charles Mzinga ilifanyika katika Usharika wa Azania Front Cathedral na kuhudhuriwa na mamia ya washarika na wageni mbalimbali waliokuwa na shauku kubwa ya kumaliza mwaka 2023 na kuingia mwaka mpya wa 2024.

Akizungumza katika ibada hiyo Dean Chediel Lwiza aliwakumbusha washarika na watu wote waliohudhuria ibada hiyo kutubu, kumrudia Mungu ili kuumaliza mwaka 2023 salama na kuanza mwaka mpya 2024 wakiwa wasafi ili kuweza kufurahia matunda ya baraka za Bwana.

“Tunapomaliza mwaka 2023 na kuingia mwaka mpya 2024 Mungu anataka tuingie kwa njia ya toba. Inawezekana katika mwaka huu tunaomaliza ilifika mahali mahusiano yako binafsi na Mungu hayakuwa mazuri, labda tulitenda dhambi, labda tuliwaza vibaya au tulifikiri vibaya. Inwezekana pia katika mwaka unaopita tulipata mali zisizo za halali. Mungu anataka tuingie mwaka 2024 kwa toba”, alisema Dean Chediel Lwiza.

Somo: 1 Samweli 7:12-17; Hata Sasa Bwana Ametusaidia.

Dean Chediel Lwiza akizungumza wakati wa ibada | Picha: AZF Media Team

---------------------------------------------------------

Washarika Azania Front katika Ibada ya Mwaka Mpya 2024

Washarika wa Azania Front walijumuika siku ya Jumatatu tarehe 01/01/2024, siku ya kwanza kabisa ya mwaka 2024 ili kumshukuru Mungu kwa neema ya kuingia mwaka mpya wa 2024.

Katika ibada hiyo iliyoongozwa na Msaidizi wa Baba Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Dean Chediel Lwiza akisaidiwa na Mchungaji Kiongozi wa Usharika, Chaplain Charles Mzinga ilifanyika katika Usharika wa Azania Front Cathedral na kuhudhuriwa na mamia ya washarika na wageni mbalimbali waliokuwa na shauku kubwa ya kuingia mwaka mpya wa 2024.

Akizungumza katika ibada hiyo Dean Chediel Lwiza aliwaasa washarika na watu wote waliohudhuria ibada hiyo kujenga utamaduni wa kuweka malengo na kutumia muda vizuri katika shughuli zao zote.

Ndugu zangu hakuna kitu kibaya duniani ambacho kikipotea huwa akirudi kinachoitwa muda. Muda siku zote hukipita, umepita. Na kutokutunza au kutumia muda vizuri ni dhambi yaani ni sawasawa na kuvunja zile amri zote kumi za Mungu. Mtu anayetumia muda vibaya anatenda dhambi sawasawa na dhambi zingine zote unazozijua”, alisema Dean Chediel Lwiza.

Nyinyi wapendwa wa Mungu, Mungu amewapa mwaka (muda) mwingine tena na anapokupa muda anataka aone utakavyotumia huo muda vizuri ili kuleta maisha ya baraka na yenye tija kwako. Tunaposema tunamshukru Mungu kwa mwaka 2024, lakini unafahamu kwamba Mungu amekupa muda? Na kwamba kwenye huo muda aliokupa unapaswa kuutumia vizuri? Wapo watu wanaolalamika kuhusu maisha yao mabaya, hayaendi. Mtu akishaanza kulalamika kuhusu maisha yake, muulize ndugu naomba uniambie namna unavyotumia muda wako kwa siku...?”, alihoji Dean Chediel Lwiza.

Somo: Luka 13:6-9; Tuanze Yote Katika Jina la Yesu

 

New Year Service at Azania Front Cathedral

Speaking in the New Years’ Service at Azania Front Cathedral Rev. Joseph Mlaki told the congregants to forget about their failures and help them focus and do more greater things in the new year 2024.

“In this year 2024, love your God and your neighbors as much as you love yourself”, said Rev. Joseph Mlaki.

Theme: Luke 13:6-9; Let Begin Everything in the Name of Jesus Christ.