Katika ibada ya mkesha wa Krismasi (Usiku Mtakatifu), siku ya kukumbuka kuzaliwa kwa mwokozi Yesu Kristo iliyofanyika tarehe 24/12/2023 kwenye Usharika wa Kanisa Kuu Azania Front na kuongozwa na Msaidizi wa Baba Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Dean Chediel Lwiza, washarika kuwa na imani na Mungu kwa kuiga mfano wa Bikira Maria ambaye alipewa habari ya uzao wa Yesu Kristo na akaamini.
“Huyu Binti wa watu (Bikira Maria) asiyemjua mtu yeyote, anapewa habari hii (ya kuzaliwa Yesu Kristo) anaamini, anaipokea. Hili sio jambo dogo. Yapo matendo ambayo unaweza kuyatenda na ukaamini kwa haraka lakini hili la kusikia habari ngumu mno na kuiamini, haikuwa kitu chepesi sana. Bikra kubeba mimba ni jambo ambalo hata sheria za asili zinashindwa kuelezea, lakini kwa imani tunaweza kuona kwamba inawezekana”.
Ndugu zangu tunapoendelea kutafakari juu ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo, tutafakari pia anavyoweza kubadilisha, kuchunga na kutawala maisha yetu.” Dean Lwiza aliongeza.
Ibada hii pia ilihudhuriwa na Mchungaji Kiongozi wa Usharika, Chaplain Charles Mzinga ambaye alishriki katika kuongoza ibada.
Dean Chediel Lwiza (katikati), Chaplain Charles Mzinga (kulia) na Mchungaji Joseph Mlaki (kushoto) wakifurahia jambo mara baada ya ibada. Picha: AZF Media Team
Christmas Eve at Azania Front Cathedral | English Service
Preaching in the Christmas Eve Service (Holy Night), the day to remember the birth of Jesus Christ Rev. Lusungu Mbilinyi told the congregants to celebrate in the presence of Jesus Christ noting that by doing so that is the only way it counts.
“As we start this Christmas season we should ask ourselves as we continue to celebrate, is Jesus himself invited to his birthday or we just only have decorated celebrative Christmas while Jesus is not present. I would like to ask you to invite Jesus Christ in your midst. He might be less fun now but I can promise you it pays having him there”, said Rev. Lusungu Mbilinyi
The service which took place at Azania Front Cathedral was also attended by Rev Joseph Mlaki who led the service proceedings.
------------------------------------------------------------
Washarika Azania Front Washerehekea Sikukuu ya Krismasi
Katika ibada ya Krismasi iliyofanyika tarehe 25/12/2022 kwenye Usharika wa Kanisa Kuu Azania Front na kuongozwa na Baba Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani Dkt. Alex Malasusa, aliwakumbusha washarika juu ya umuhimu na ukubwa wa sikukuu ya Krimasi na umuhimu wake katika maisha ya wanadamu.
“Ndugu zangu leo ni siku kubwa sana duniani, siku hii ya Krismasi, siku ambayo inagusa mamilioni ya watu katika ulimwengu huu. Watu wengi wanaofuatilia sikukuu mbalimbali duniani watakubaliana na mimi kwamba hakuna sikukuu inayosherehekewa na watu wengi tena bila kujali tabaka, tamaduni, mataifa mbalimbali, lugha mbalimbali, wote wanasherehekea Krismasi. Ni siku ya pekee sana, haijalishi hata mtu ana dini gani, lakini atasherehekea Krismasi”, alisema Baba Askofu.
“Haijalishi umerukaruka kiasi gani, lakini ukiomba kwa imani anasikia kwa kuwa Mungu tunayemwamini na kwa njia hii ya Yesu Kristo kuzaliwa kwake, Mungu anafanyika kuwa Emmanuel yaani Mungu pamoja nasi.Mungu hayuko mbali, ni sisi tu kufungua mioyo yetu ili Yesu anayezaliwa, azaliwe mioyoni mwetu,” alisema Baba Askofu.
“Bahati mbaya sana wakristo wengi hatusherehekei Krismasi kwa faida, tunasherehekea kwa hasara. Mwaka mzima wa kanisa unakuwa hasara. Hata siku ya kuzaliwa Yesu Kristo bado tunaiona kama maadhimisho, ndugu zangu leo sio maadhimisho bali Mungu anatukumbusha kupitia mwaka wake wa kanisa kuwa ni lazima Yesu azaliwe katika maisha yetu na katika mioyo yetu”. aliongeza Baba Askofu.
Somo: Yohana 1:1-5; Kwa Ajili Yetu Mwokozi Amezaliwa Haleluya.
Ibada hiyo pia ilihudhuriwa na Msaidizi wa Baba Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Dean Chediel Lwiza pamoja na Mchungaji Kiongozi wa Usharika, Chaplain Charles Mzinga.
Celebrating Christmas at Azania Front Cathedral | English Service
Preaching in the Christmas Service, the day to remember the birth of Jesus Christ Rev. Lusungu Mbilinyi reminded the congregation that by the birth of Jesus Christ, God wanted to be closer to us and guide us throughout our lives.
“Jesus came into this life to have a fellowship with you”. Dear congregants, I welcome you, when you are sitting in this day on the Christmas table enjoying your Christmas meal, to invite Jesus Christ to be on that table too”, said Rev. Lusungu Mbilinyi
The service which took place at Azania Front Cathedral was also attended by Rev Joseph Mlaki who led the service proceedings.