MATANGAZO YA USHARIKA 

TAREHE 03 DISEMBA, 2023

SIKU YA BWANA YA KWANZA KATIKA MAJILIO

NENO LINALOTUONGOZA NI

BWANA ANALIJIA KANISA LAKE

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia kwa cheti. 

3. Matoleo yaTarehe 26/11/2023

4. Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 mchana. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV. 

6. Leo tarehe 03/12/2023 tutamtolea Mungu fungu la kumi. Washarika Karibuni.

7. Kwaya Kuu ya Usharika inapenda kuwataarifu Washarika kuwa Thermos na Diary tayari vimeshafika. Wale waliokosa na pia wanaotaka kuongeza zingine wanakaribishwa sana jumapili ijayo tarehe 10/12/2023 vitauzwa katika ibada zote, Thermos itauzwa kwa bei ya elf 30 na Diary elf 15. Wanaomba Washarika muweze kuwaunga mkono ili kutunisha mfuko wao. Pia siku hiyo Kwaya ya Agape watauza Kalenda za Mwaka 2024. Mungu awabariki sana.

8. Uongozi wa umoja wa vijana unapenda kuwatangazia vijana wote na wale wanaopenda kuigiza kufika kwenye zoezi siku ya Jumatatu saa kumi na moja jioni na jumamosi saa tisa alasiri Kwa ajili ya maandalizi ya igizo la krismasi. Mungu awabariki

9. SHUKRANI: JUMAPILI IJAYO TAREHE 10/12/2023

IBADA YA KWANZA SAA 1.00 ASUBUHI

  • Familia ya Chris Rabi watamshukuru Mungu kwa mambo mema mengi aliyowatendea

Neno: Zaburi 9:1-2, Wimbo: TMW 295 (Mungu amenihurumia)

  • Familia ya Steven na Vicky Katikaza watamshukuru Mungu kwa kutimiza miaka 20 ya ndoa tarehe 06/12/2023, kuwapa ulinzi, Zawadi ya motto wa kike pamoja na mambo mengi aliyowatendea.

Neno: Mith 19:14, Wimbo: TMW 175 (Heri kumjua Yesu Bwana)

  • Familia ya Marehemu David Urio wanamshukuru Mungu kwa mema mengi aliyowatendea ikiwa ni pamoja na kuwapigania na kuwafanikisha katika kazi na biashara. Pia wanamshukuru Mungu kwa kijana wao Davis kufunga ndoa takatifu October 7 mwaka huu. 

Neno kutoka Zaburi 138:1-3 na wimbo namba 295.

IBADA YA TATU SAA 4.30 ASUBUHI

  • Familia ya Marehemu Rabian na Nsia Kimaro Watamshukuru Mungu kwa kuwasimamia, kuwapigania kwa fadhili zake na Upendo wake aliowaonesha kwa kipindi chote cha kuondokewa na Mama yao mpendwa mwaka mmoja uliopita.

Neno: Zaburi 91:2, Zaburi 27:13,Kumb. 31:8, Wimbo: TMW 49

  • Familia ya Marehemu Diaz Matoi nao watamshukuru Mungu kwa mambo mengi aliyowatendea katika maisha yao ikiwa ni pamoja na kumaliza salama msiba wa mpendwa wao Mzee Diaz Matoi.

Neno: Nahumu 1:7, Wimbo: TMW 173

9. Jumapili ya tarehe 31/12/2023 Kundi la Waliozaliwa mwezi wa Desemba Kwaya Kuu, watatoa Shukrani ya pekee katika ibada ya tatu saa 4.30 asubuhi, Pia wanatoa mwaliko kwa washarika wote Waliozaliwa Desemba kuungana nao kumshukuru Mungu Kwa mambo Makuu aliyowatendea”

10. NDOA ZA WASHARIKA

MARA YA PILI TUNATANGAZA NDOA YA TAREHE 16/12/2023 

SAA 08:00 MCHANA

  • Bw. Wilbert Exaud Kwayu na Bi. Simona Mrinji Gadi 

SAA 9.00 ALASIRI

  • Bw. Modest Mero na Bi. Vicky Kawedi Shayo

MARA YA TATU TUNATANGAZA NDOA YA TAREHE 09/12/2023 

SAA 07:00 MCHANA

  • Bw. Nguzo Heriel Kida na Bi. Catherine Ngarami Mushi 

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo.

11. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

  • Oysterbay na Masaki: Kwa Bwana na Bibi Stephen Katikaza.
  •  
  • Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Bwana na Bibi Charles Lyimo
  •  
  • Mjini kati: Watatangaziana
  •  
  • Ilala, Chang’ombe na Buguruni: Kwa Dada Elipenda Mkandawire
  • Kinondoni: Kwa Mama Hilda Lwezaura
  • Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bwana Allen David
  • Upanga: Kwa Bwana na Bibi George Kinyaha 

12. Zamu: Zamu za wazeeni ni kundi la Pili.

Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.