Date:
30-11-2023
Reading:
Matendo 24:15-16
Alhamisi asubuhi tarehe 30.11.2023
Matendo ya Mitume 24:15-16
15 Nina tumaini kwa Mungu, ambalo hata hao nao wanalitazamia, ya kwamba kutakuwa na ufufuo wa wafu, wenye haki na wasio haki pia.
16 Nami ninajizoeza katika neno hili niwe na dhamiri isiyo na hatia mbele za Mungu na mbele ya watu siku zote.
Maandalizi kwa uzima wa milele;
Kazi ya kuhubiri Injili haikuwa nyepesi kwa Mtume Paulo na wenzake. Katika somo tulilosoma, ni Mtume Paulo akiwa mbele ya liwali anajitetea, maana Kuhani Mkuu Anania aliwaongoza wenzake kumshtaki mbele ya Liwali. Paulo anashtakiwa kwa kufundisha kinyume na imani ya Kiyahudi.
Akijitetea, Mtume Paulo hakuikana imani. Aliendelea kumkiri Yesu. Anasema analo tumaini katika ufufuo wa wafu, na anaamini katika huo ufufuo ili asiwe na hatia.
Kumbe ufufuo upo kwa wote walioiamini kweli ya Kristo. Tujiandae kuingia mbinguni tukimkiri Kristo kwa matendo yetu. Amina
Alhamisi njema.
Heri Buberwa