Date: 
22-11-2023
Reading: 
Mathayo 13:36-43

Jumatano asubuhi tarehe 22.11.2023

Mathayo 13:36-43

36 Kisha Yesu akawaaga makutano, akaingia nyumbani; wanafunzi wake wakamwendea, wakasema, Tufafanulie mfano wa magugu ya kondeni.

37 Akajibu, akasema, Azipandaye zile mbegu njema ni Mwana wa Adamu;

38 lile konde ni ulimwengu; zile mbegu njema ni wana wa ufalme; na yale magugu ni wana wa yule mwovu;

39 yule adui aliyeyapanda ni Ibilisi; mavuno ni mwisho wa dunia; na wale wavunao ni malaika.

40 Basi, kama vile magugu yakusanywavyo na kuchomwa motoni; ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia.

41 Mwana wa Adamu atawatuma malaika zake, nao watakusanya kutoka katika ufalme wake machukizo yote, na hao watendao maasi,

42 na kuwatupa katika tanuru ya moto, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.

43 Ndipo wenye haki watakapong'aa kama jua katika ufalme wa Baba yao. Mwenye masikio, na asikie.

Hukumu ya mwisho inakuja;

Wanafunzi wanamuomba Yesu awaambie maana ya mfano wa magugu ya kondeni. Mfano huu Yesu aliutoa hapo kabla kama tunavyoweza kuurejea;

Mathayo 13:24-26

24 Akawatolea mfano mwingine, akisema, Ufalme wa mbinguni umefanana na mtu aliyepanda mbegu njema katika konde lake;
25 lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake.
26 Baadaye majani ya ngano yalipomea na kuzaa, yakaonekana na magugu.

Kwa hiyo somo la asubuhi hii ni jibu la mfano huo. Kwamba apandaye mbegu njema ni Yesu Kristo, konde ni ulimwengu, mbegu njema ni kundi la waaminio, magugu ni wasioamini. Adui ni ibilisi, mavuno ni mwisho wa dunia, wavunao ni malaika.

Yesu anaonesha nafasi yake kama Mwokozi wa ulimwengu, kwamba kwa njia ya imani na neno lake, basi waaminio wote na kuishi kwa neno lake wataurithi uzima wa milele. Amina.

Jumatano njema.

Heri Buberwa