MATANGAZO YA USHARIKA
TAREHE 05 NOVEMBA, 2023
SIKU YA KUKUMBUKA WATAKATIFU
NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI
UENYEJI WA MBINGUNI
1.Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia kwa cheti.
3. Matoleo ya Tarehe 29/10/2023
Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.
NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:
0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT
Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL
4. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 mchana. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV.
5. Kamati ya Afya na Ustawi wa jamii inapenda kuwatangazia kuwa mafundisho ya afya kwa wanafunzi wa Kipaimara kwa mwaka wa Kwanza na wa pili yatafanyika tarehe18/11/2023 kuanzia saa 2.30 asubuhi mpaka sa 8.00 mchana hapa Usharikani. Wale waliopata Kipaimara kuanzia miaka 3 iliyopita wanakaribishwa kwenye mafundisho haya. Sambamba na Elimu ya Afya kwa Wanafunzi hao Wazazi na Walezi pia watakuwa na muda wa kujadili juu ya changamoto Malezi ya Watoto. Wazazi na Walezi mnaombwa kujiandikisha na kuandikisha Watoto watakaohudhuria kwa Parish Worker ili kufanya maandalizi haya.
6. Leo tarehe 05/11/2023 tutamtolea Mungu fungu la kumi. Washarika karibuni.
7. Jumamosi ijayo tarehe 11 Novemba 2023 kutakuwa na Semina ya Wajane na Wagane itakayofanyika Mtaa wa Mvuti. Usafiri utaondoka hapa Kanisani saa 1.00 asubuhi. Karibuni sana.
SHUKRANI:
Jumapili ijayo tarehe 12/11/2023 katika ibada ya tatu saa 4.30 asubuhi
- Familia yaMzee Arnold Kilewo watamshukuru Mungu kwa mambo makuu aliyowatendea ikiwa ni Pamoja na Mzee Arnold kufikisha miaka 85.
7. Jumapili ijayo tarehe 12/11/2023 ni siku ya ubatizo wa Watoto wadogo na kurudi kundini. Watakaohitaji huduma hii wafike ofisini kwa Mchungaji.
8. NDOA ZA WASHARIKA
MARA YA KWANZA TUNATANGAZA NDOA YA TAREHE 25/11/2023
SAA 09:00 ALASIRI
- Bw. Peres Peter Meena na Bi. Aneth Anase Monyo
MARA YA PILI TUNATANGAZA NDOA YA TAREHE 18/11/2023
SAA 08:00 MCHANA
- Bw. Gerald Happygod Minja na Bi. Janet Japhet Malasusa
KWA MARA YA TATU TUNATANGAZA NDOA YA TAREHE 11/11/2023
SAA 08:00 MCHANA
- Bw. Isaya Henry Shekifu na Bi. Agnes Joh Londo
Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo.
9. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA
- Oysterbay na Masaki: Kwa Mama Nisile Mollel
- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Mama Mamkwe
- Mjini kati: Watatangaziana
- Ilala, Chang’ombe na Buguruni: Kwa Bwana na Bibi Kelvin
- Kinondoni: Kwa Prof. Geofrey Mmari
- Upanga: Kwa Mama Ndossi
- Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach: Kwa Bwana na Bibi Kakuyu
10. Zamu: Zamu za wazeeni ni Pili.
Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.