Date: 
26-10-2023
Reading: 
Mathayo 11:25-30

Alhamisi asubuhi tarehe 26.10.2023

Mathayo 11:25-30

25 Wakati ule Yesu akajibu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga.

26 Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyopendeza mbele zako.

27 Akasema, Nimekabidhiwa vyote na baba yangu; wala hakuna amjuaye Mwana, ila Baba; wala hakuna amjuaye Baba, ila Mwana, na ye yote ambaye Mwana apenda kumfunulia.

28 Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.

29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;

30 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.

Tuheshimu wito tuliopewa na Mungu;

Yesu anashukuru kwa Mungu kuwapa ufunuo wote waaminio, yaani wote waliompokea na kumwamini. Kwa tafsiri nyingine maneno haya ya kuwaficha wenye hekima na kuwafunulia watoto wachanga ni maelekezo kuwa imani ya kweli ni kwa Yesu Kristo. Ndiyo maana katika mstari wa 27 Yesu anasema amekabidhiwa vyote na Baba, na yeye ndiye apaswaye kuabudiwa. Hivyo Yesu anajitambulisha kama Mungu kweli astahiliye kuaminiwa na kuabudiwa.

Ndipo anatupa ujumbe wa kumfuata yeye (28) anaposema njooni kwangu ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo nami nitawapumzisha. Anaongeza kwamba jitieni nira yangu mjifunze kwangu, kwa maana yeye ni mpole na mnyenyekevu. 

Huu ni wito wa kumfuata Yesu.

Tuheshimu wito huu. Amina

Alhamisi njema.

Heri Buberwa