Date: 
13-10-2023
Reading: 
2 Wafalme 13:34-41

Ijumaa asubuhi tarehe 13.10.2013

2 Wafalme 17:34-41

34 Hata siku hii ya leo hufanya sawasawa na kawaida za kwanza; wala hawamwogopi Bwana, wala hawazifuati sheria zao, wala hukumu zao, wala ile torati, wala ile amri Bwana aliyowaamuru wana wa Yakobo, ambaye alimpa jina la Israeli;

35 hao ambao Bwana alifanya agano nao, akawaamuru, akasema, Msiche miungu mingine, wala kuisujudia, wala kuitumikia, wala kuitolea sadaka;

36 ila yeye Bwana, aliyewaleta kutoka nchi ya Misri kwa nguvu nyingi, na kwa mkono ulionyoshwa, yeye ndiye mtakayemcha, yeye ndiye mtakayemsujudia, yeye ndiye mtakayemtolea sadaka;

37 na sheria, na hukumu, na torati, na amri, alizowaandikia, hizo ndizo mtakazozishika na kuzifanya hata milele; wala msiche miungu mingine.

38 Na hilo agano nililofanya nanyi, msilisahau; wala msiche miungu mingine;

39 lakini Bwana, Mungu wenu, ndiye mtakayemcha; naye atawaokoa mikononi mwa adui zenu wote.

40 Walakini hawakusikia, bali wakafanya sawasawa na kawaida zao za kwanza.

41 Basi mataifa hawa wakamcha Bwana, tena wakaziabudu sanamu zao za kuchongwa; na wana wao vile vile, na wana wa wana wao; kama walivyofanya baba zao, wao nao hufanya vivyo hivyo hata leo.

Uhuru wa Mkristo;

Ni ujumbe kwa wana wa Israel kumcha Bwana baada ya kukombolewa toka utumwani. Wanaamriwa kumsujudia Bwana na kumtolea sadaka. Pia wanaamriwa kushika hukumu, torati na amri za Bwana, wasiiche miungu mingine. 

Ulikuwa ni utaratibu wa kawaida wakati ule watu kuishi kwa torati. Watu walitakiwa kufuata ipasavyo, kinyume na hapo ni hukumu. Sisi leo tunaishi kwa imani katika Yesu Kristo, ambaye hutupa neema ya kuyaweza mambo yote katika yeye. Mwamini Yesu uokolewe. Amina.

Ijumaa njema 

 

Heri Buberwa 

Mlutheri