Date: 
28-07-2023
Reading: 
Methali 19:15-19

Ijumaa asubuhi tarehe 28.07.2023

Mithali 19:15-16

15 Uvivu humtia mtu katika usingizi mzito; Na nafsi yake mvivu itaona njaa.

16 Yeye aihifadhiye amri huihifadhi nafsi yake; Bali yeye asiyeziangalia njia zake atakufa.

Uchaguzi wa busara;

Asubuhi ya leo tunasoma juu ya uvivu. Tunasoma kwamba uvivu humfanya mtu kuwa na usingizi mzito. Kwa sababu ya usingizi mzito hawezi kufanya kazi, hivyo hawezi kupata chakula, hivyo kuona njaa. Lakini pia tunasoma juu ya kuhifadhi nafsi kwa mtu yule azishikaye amri za Mungu. Asiyezishika amri mwisho wake kufa!

Katika Mithali hizo hapo juu, tunaposoma juu ya uvivu tutafakari katika dhana pana ya kutokuwajibika. Yaani uvivu wa kutofanya kazi, lakini pia na kutolishika neno la Mungu. Ndiyo maana mstari wa 16 unasisitiza kuzishika amri, yaani kutokuwa mvivu katika kumfuata Kristo. Tunapolishika neno la Mungu na kuzishika amri zake hapo ndipo tunakuwa tumefanya Uchaguzi wa busara. Ubarikiwe 

 

Heri Buberwa