Date: 
21-07-2023
Reading: 
1Yohana 4:7-10

Ijumaa asubuhi tarehe 21.07.2023

1 Yohana 4:7-10

7 Wapenzi, na mpendane; kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu, na kila apendaye amezaliwa na Mungu, naye anamjua Mungu.

8 Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo.

9 Katika hili pendo la Mungu lilionekana kwetu, kwamba Mungu amemtuma Mwanawe pekee ulimwenguni, ili tupate uzima kwa yeye.

10 Hili ndilo pendo, si kwamba sisi tulimpenda Mungu, bali kwamba yeye alitupenda sisi, akamtuma Mwanawe kuwa kipatanisho kwa dhambi zetu.

Amri ya Upendo;

Yohana analiandikia Kanisa kupendana maana pendo latoka kwa Mungu, na kila apendaye amezaliwa na Mungu, anamjua Mungu. Asiyependa hamjui Mungu maana Mungu ni upendo! 

Yohana anasisitiza kwamba sisi hatukumpenda Mungu, bali yeye alitupenda akamtuma Yesu kufa na kutupatanisha kwa Baba. Upendo wake ni dhahiri.

Pendo litokalo kwa Mungu limetufanya tulivyo, yaani kuokolewa. Kumbe maisha tunayoishi ni kwa sababu ya pendo la Mungu. Sasa pendo hili la Mungu lionekane kwetu kwa kupendana. Yaani kama kweli tumetokana na pendo lake, basi tupendane. Upendo kati yetu humtangaza Kristo aliye Upendo, hivyo tupendane. Amina.

Ijumaa njema.

 

Heri Buberwa