MATANGAZO YA USHARIKA 

TAREHE 9 JULY, 2023

NENO LINALOTUONGOZA NI

MTU AKINITUMIKIA NA ANIFUATE 

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia kwa cheti. .

3. Matoleo ya Tarehe 02/07/2023

4. Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 -7.30 mchana tunapopata faragha binafsi na Mungu. Alhamisi jioni saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV. 

6. Kwaya ya Agape wanapenda kuwakaribisha washarika wote na waimbaji wa vikundi vyote kushirikiana nao kwenye maandalizi ya Tamasha la Uinjilisti Pamoja na safari ya Injili Mwanza. Siku za mazoezi ni Jumatano saa 11.00 jioni, Jumamosi saa 6.00 Mchana na Jumapili baada ya ibada ya kwanza.

7. NDOA. NDOA ZA WASHARIKA

NDOA IFUATAYO ITAFUNGWA KATIKA KANISA LA MTAKATIFU PETRO OYSTERBAY TAREHE 29.07.2023,

  • KWA MARA YA KWANZA TUNATANGAZA NDOA HII KATI YA BWANA FRANK MARTIN MOLLEL NA BI MIRIAM ALEX MALASUSA
  •  
  • KWA MARA YA TATU TUNATANGAZA NDOA YA TAREHE 15/07/2023, NDOA HII ITAFUNGWA KANISA KUU LA MTAKATIFU JOSEPH DAR ES SALAAM
  • Bw. Deogratias Alfred Mboya na Bi. Sianael Obedy Shoo

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo.

8. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

  • Oysterbay na Masaki: Kwa BWANA NA BIBI DAVID MOLLEL
  • Ilala, Chang’ombe na Buguruni: BW & BI JAMES MONYO 
  • Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: KWA BW & BI MWAITEMBO
  • Upanga:KWA BW & BI SABAYA
  • Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach: BW & BI HENRY MWANYIKA
  • Tabata: KWA MCHUNGAJI KIBONA
  • English Service: BW & BI CHOMBA 

9. Zamu: Zamu za wazeeni Kundi la Kwanza.

Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.