Date: 
28-06-2023
Reading: 
Warumi 7:4-6

Jumatano asubuhi tarehe 28.06.2023

Warumi 7:4-6

4 Kadhalika, ndugu zangu, ninyi pia mmeifia torati, kwa njia ya mwili wa Kristo, mpate kuwa mali ya mwingine, yeye aliyefufuka katika wafu, kusudi tumzalie Mungu matunda.

5 Kwa maana tulipokuwa katika hali ya mwili, tamaa za dhambi, zilizokuwako kwa sababu ya torati, zilitenda kazi katika viungo vyetu hata mkaizalia mauti mazao.

6 Bali sasa tumefunguliwa katika torati, tumeifia hali ile iliyotupinga, ili sisi tupate kutumika katika hali mpya ya roho, si katika hali ya zamani, ya andiko.

Neema ya Mungu yatuwezesha;

Mtume Paulo anawapongeza Warumi kwa kumwamini Kristo mfufuka, aliyewaokoa toka dhambini kwa njia msalaba. Anawapongeza kwa kuacha hali ya mwili waliyokuwa nayo kwa njia ya torati. Anawahimiza kudumu katika Kristo Yesu aliye Mwokozi wa Ulimwengu, kwa njia ya imani

Ujumbe huu unatujia sisi asubuhi hii ukitukumbusha kuwa baada ya kuja kwa Yesu hatuko chini ya sheria, bali tumeokolewa kwa neema. Hatuko chini ya sheria, bali Yesu Kristo hutuongoza na kutuwezesha katika yote kwa neema yake. Dumu katika neema hii kwa kumwamini Yesu. Amina.

Siku njema.

Heri Buberwa